Siku ya Kwanza Kula tikiti maji

Siku ya Kwanza Kula tikiti maji

Juzi hapa nilimlazimisha rafiki yangu kula parachichi. Alikuwa hajawahi kula kabla ya hapo. Sasa kila nikimshawishi alikuwa hataki. Nikakata kipande kidogo hivi cha pembe tatu.

Nikamwambia kula hata hucbi kidogo huku usilifikirie, jamaa akala.

Aiseeh. Unajua alisemaje

"Kuna kipande chengine hapo uniongeze".

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili tunda nlinunuaga nkala nlishindwa kumaliza kipande kimoja nkalitupa ila sijui nimelizoea vipi bhana leo hii mawili hayawezi nitosha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili huwa naliona kwenye mavitabu ya kizungu tu, siku nikiliona lazima nilionje pia. Haiwezekani mwaka mzima unakula matunda aina nne au tano tu, labda ndio maana akili zinakuwa za kuungaunga.

😂😂😂yaan ww unanichekeshaga kuanzia jina lako had unachoandika..dah hapa kichwa kinauma ila nimecheka tu
 
Naona kama nitalitapika!!.. Ingawa nitakuja jitosa siku moja nilijaribu kama nilivyoweza jitosa Sambusa na Supu!..

😂😂😂😂hupend supu?sambusa?dah
Tikiti maji kama nikialikwa ugenini ndio nakula kwa McHale nisimkwaze mwenyeji, nyumbani siligusi. Parachichi ikiwa juice nitajihidi kunywa.

Sent using Jamii Forums mobile app

upo km mm ...
 
Mie nakumbuka ilikua 2004 huko rombo.....tulikua tumetoka mafundisho ya dini bhana....tukawa tunapita mashambani tukakuta madude hata hatuyaelewi....at the first tulidhani ni maboga...tukalichukua tukalivunja ndani tukakuta lipo tofauti na boga....tukaonja mara tamu kichizi yani...acha tuyafakamie sasa hofu ikaje...tulikua tunahofia tusijekuwa tumekula lile tunda lililokatazwa kwenye bustani...tulikua tunasubiria kufa maana matumbo yalivimba kw maji mengi...ila baada ya masaa kupita tuko fresh ndio baadae tukaja kuambiw ni matikiti

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla sijacomment naomba kuuliz.. Hivi yanayozungumziwa humu ni matunda au ni vitu vingine
 
Sijawahi onja fenesi kabisaaa, na sijui kama nitakujaga kulionja!
Tango nalo mie kulila ni mtihani
 
Mie nakumbuka ilikua 2004 huko rombo.....tulikua tumetoka mafundisho ya dini bhana....tukawa tunapita mashambani tukakuta madude hata hatuyaelewi....at the first tulidhani ni maboga...tukalichukua tukalivunja ndani tukakuta lipo tofauti na boga....tukaonja mara tamu kichizi yani...acha tuyafakamie sasa hofu ikaje...tulikua tunahofia tusijekuwa tumekula lile tunda lililokatazwa kwenye bustani...tulikua tunasubiria kufa maana matumbo yalivimba kw maji mengi...ila baada ya masaa kupita tuko fresh ndio baadae tukaja kuambiw ni matikiti

Sent using Jamii Forums mobile app

😂😂😂
 
Kuna tunda linaitwa kiwi... Natamani siku nlionje.. But hisia zangu zinaniambia lina ladha mbaya kuliko matunda yote

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama uko Daslam tembelea soko la food lovers masaki utalipata au uhindini ila moja tsh elf tatu. Huku nilipo yako mengi tena bei chee....

Ni matamu mnoo na yana virutubisho vingi mwilini. Nayapenda sana.

4000B3FC-ABF1-4AB2-B0A6-C9D9D7A76588.jpeg

Hizo nyingine ni zabibu zisizo na mbegu, ni tamu mnoo.

I love eating 😋.

Kasie.
 
Basi mi nkiyaangalia na huo ukijani wake napata picha ladha ni ya ugwadu halafu ya ajabu
Kama uko Daslam tembelea soko la food lovers masaki utalipata au uhindini ila moja tsh elf tatu. Huku nilipo yako mengi tena bei chee....

Ni matamu mnoo na yana virutubisho vingi mwilini. Nayapenda sana.

View attachment 1008164

Hizo nyingine ni zabibu zisizo na mbegu, ni tamu mnoo.

I love eating [emoji39].

Kasie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom