Qwy
JF-Expert Member
- Nov 23, 2018
- 6,238
- 31,190
Nadhani kwenye hili kila mtu analichukulia kinamna yake, nimeona maiti kadhaa, nimeshiriki kuosha maiti lakini huwa nikitoka hapo nayaacha huko huko.Hakika kila nafsi itaonja mauti japo kifo hakizoeleki kabisa ndo maana huwa tunaumia sana tukifiwa.
Kuna siku niliona maiti ya mmama aliegongwa na gari nikiwa la saba aisee ile picha haijawahi potea kichwani mwangu ubaya alikuwa bado amefungua macho[emoji24][emoji24][emoji24] Baada ya lile tukio alifariki rafiki yangu hakika sikuweza kwenda kuaga nilishindwa kabisa! Mungu awalaze mahali pema peponi.
Je siku ya kwanza kuona maiti ilikuwaje?? Hii memory ni mimi tu nashindwa kuifuta au?