educator2025
JF-Expert Member
- Dec 24, 2013
- 395
- 455
Wandugu kama mjuavyo wengi wetu tumesoma shule za st. Kayumba kwa hiyo Ngeli ni ishu kwetu. Basi kwa kuunga unga hivyo hivyo nikachaguliwa Chuo (UDSM) sasa kufika huko si ndo mambo ya Seminar za DS 101 natakiwa ni-present ilikuwa balaa usiku kabla ya seminar sikulala naogopa.
Kwenye seminar yenyewe sasa jasho lilinitoka mwili mzima balaa yaani naona nyota nyota tu daah! sitaki kukumbuka. Lakini namshukuru Mungu baada ya pale nilifanya bidii y kujifunza kwa kusoma zaidi vitabu vya kiingereza na kuongea na watu wasiojua kiswahili (hasa waganda, Wazambia & Waganda).
Angalau sasa mambo si mabaya Ulimi si mzito tena kiviile!!! English aisee ni hatari jamani. SHIKAMOO KIINGEREZA
**Halafu mademu wanazingua mno, ukikosea wanakucheka balaa daah. Ukiwa na demu chuo ni shidaa sana