Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Kuna mmoja tukiwa form one wakati huo kulikuwa na 'no English no service' rule, siku hiyo jamaa alisahau daftari, mwalimu kafika kwa mwanafunzi aliyekuwa mbele ya huyo jamaa, akaulizwa where is your exercise book akajibu I forgot it home, sasa ilipofika za much yake hakujua yule jamaa wa mbele alisemaje, alipoulizwa akasema I dolilo. Class nzima ilipasukiwa na kicheko
 
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana
Hahahaaaa, mkuu kitu cha Prof. Mlambiti nn?
 
Mimi nakumbuka tulikuwa tunawasilisha seminar ya IT. Swali lilikuwa "what is folder" hapo tupi first year. Mwasilishaji alitafuta maneno yote yakagoma kuja japo alimeza usiku mzima. Gafla akajibu folder is like a kabati, where there are cups, plates and so on" alipomaliza jasho lilikuwa linamtoka balaa. Ikabid mwl. amwambie kakae. Kiingereza si mchezo.
 
Ha ha ha ha ha ha mbavu zangu miee......sema sio mbaya..tunajifunza kulingana na makosa...I go,I come. why because
 
Nakumbuka miaka ya nyuma nilishawahi kwenda Interview ya Bank Teller CRDB pale Azikiwe daah sijui ndo kiingereza au uoga maana nilikuwa nikiulizwa swali najibu kwa sauti kubwa kama napiga ADHANA MSIKITINI (Swalaa Swalaa saa 11 alfajiri) mpaka yule HR akaniambia ndugu hebu RELAX hiii sio vita!! si unajua tena umemaliza shule umekaa mtaani kazi huna ghafla uaitwa interview wee nilikremu vitu balaa kufika tu mi natapika hata nisivyoulizwa

Hahaha dah aisee naonekana chizi huku kwa kucheka
 
Back
Top Bottom