Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wandugu kama mjuavyo wengi wetu tumesoma shule za st. Kayumba kwa hiyo Ngeli ni ishu kwetu. Basi kwa kuunga unga hivyo hivyo nikachaguliwa Chuo (UDSM) sasa kufika huko si ndo mambo ya Seminar za DS 101 natakiwa ni-present ilikuwa balaa usiku kabla ya seminar sikulala naogopa, kwenye seminar yenyewe sasa jasho lilinitoka mwili mzima balaa yaani naona nyota nyota tu daah! sitaki kukumbuka. Lakini namshukuru Mungu baada ya pale nilifanya bidii y kujifunza kwa kusoma zaidi vitabu vya kiingereza na kuongea na watu wasiojua kiswahili (hasa waganda, Wazambia & Waganda) Angalau sasa mambo si mabaya Ulimi si mzito tena kiviile!!! English aisee ni hatari jamani. SHIKAMOO KIINGEREZA
I want to question u, what is Biology?
I sawed the results, i passed away
Kuna mmoja tukiwa form one wakati huo kulikuwa na 'no English no service' rule, siku hiyo jamaa alisahau daftari, mwalimu kafika kwa mwanafunzi aliyekuwa mbele ya huyo jamaa, akaulizwa where is your exercise book akajibu I forgot it home, sasa ilipofika za much yake hakujua yule jamaa wa mbele alisemaje, alipoulizwa akasema I dolilo. Class nzima ilipasukiwa na kicheko
Siku moja tupo kwenye seminar ya koz moja inaitwa rural agricultural economy maarufu kama YELLOW BOOK kwa waliosoma SUA wataelewa, basi picha moja ilikua imebandikwa ukutani ikapulizwa upepo ikadondoka chini jamaa kule mbele akiwa na maiki alisema "what is that, ooh the picture drop down without becouse" basi tulicheka sana
Katika presentation ya kudefend dissertation chuon, Inatakiwa kubadilisha sehemu ya research proposal kua past tense, then ndo uje kuendelea na Part ya Result and discusion. Hivyo watu wanaweka was, were za kutosha. Bas mdada ananza kuwasilisha pale, "Goodmorning, My name WAS xxxx"
Yani hata yeye hakuamini alichokisema.
Mie nakumbuka form one Kantalamba,nimefika nikawa kiranja,basi nikashika zamu kuongoza assemble,tumeimba nyimbo zote,ikafika muda wa kuwatawanyisha nikasema "you may disappear" badala "you may dispace" basi ilikuwa gumzo. Ticha akaniita chemba kunielekeza umombo. Ha ha ha
hiz kura pia noma, kama kuna ticha mmoja wakati tupo o level walikuja wazungu kutoka marekani walileta vitabu, walimu wakawa wanajitambulisha paredi, maadam mmoja alisema 'my name is madaam sanga, am married by two childrens'