Nakumbuka siku ya kwanza kuongea kiingereza nipo shule ya msingi kayumba,kihome kulikuwa na mabroo muda wote walikuwa wanaongea kidhungu,aisee kuna swali nilimuuliza kaka mmoja kwa kidhungu alinikatisha sana tamaa,alinicheka akaniambia eid kingereza hakiongelewi ivo dah....!!!! Nilikuwa mdogo sana,nikamkataa huyo jamaa nikajipendekeza kwa marafiki zake wengine wawili ambao kwa sasa ni marehemu,nashukuru sana ndo walikuwa waalimu wangu wakubwa wa kiingereza,mara home akapanga broo mmoja alikuwa anasoma mlimani lakini huwa likizo anaenda zambia kwa bimkubwa wake hapo nipo kidato cha kwanza alikuwa wakati wote akiniongelesha kidhungu na alikuwa akinishanga kayumba nipo kidato cha kwanza nilikuwa nakinyosha ,akawa ananikubari anasema mlimani pale chuoni kuna jamaa zake kibao hata kuunda sentesi nyepesi ambayo ipo sahh ni tatizo,aise nashukuru kwa kiasi fulani jamaa amenijenga sanaaa........ilikuwa kama hatupo bongo vile,kun madada fulan wa kikenya na america nikiongea nao wananiambia aiseee upo vizuri sana lakini huwa najiona bado kabisaa