Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Siku ya Kwanza Kuongea Kiingereza mbele ya Kadamnasi kidogo nizimie

Nakumbuka miaka ya nyuma nilishawahi kwenda Interview ya Bank Teller CRDB pale Azikiwe daah sijui ndo kiingereza au uoga maana nilikuwa nikiulizwa swali najibu kwa sauti kubwa kama napiga ADHANA MSIKITINI (Swalaa Swalaa saa 11 alfajiri) mpaka yule HR akaniambia ndugu hebu RELAX hiii sio vita!! si unajua tena umemaliza shule umekaa mtaani kazi huna ghafla uaitwa interview wee nilikremu vitu balaa kufika tu mi natapika hata nisivyoulizwa
😂😂😂
 
Mie nakumbuka form one Kantalamba,nimefika nikawa kiranja,basi nikashika zamu kuongoza assemble,tumeimba nyimbo zote,ikafika muda wa kuwatawanyisha nikasema "you may disappear" badala "you may disperse" basi ilikuwa gumzo. Ticha akaniita chemba kunielekeza umombo. Ha ha ha
We mjuba kwamba wapotee🤣
 
We mtoa bandiko utakuwa umetumwa wewe siyo bure

We achana na DS ya akina dokta kamata, bwana ee, kuna ishu inaitwa principals of accounting, kuna lect anaitwa masoud aliingia kufundisha kwa mara ya kwanza, kiingereza chake unasikia maneno mawil tu debit side na credit side...mengne yote unasikia ng,ocho ng'ochooo
NIKAWAAMBIA WENZANGU TURUDI TU HOME HAPA TUMEISHA DISCO...mambo ya chuo ni upuuzi kweli kweli
 
Siku moja ndio ilikua Mara yangu ya kwanza kuzungumza kingereza ujue jamii ambayo natokea ukiwa unazungumza kingereza unaonekana unajidai unajimwambafy...SO KINGEREZA KILIKUA KIME BE ABOLISHED PALE MASOMONI ☺️😅
Sana Sana pale shuleni ilitumika CODE MIXING

Nikiwa shule Mimi na jamaa mmoja akaniingiza matatizoni.. mwalimu akatuita nikajieleza wee kwa kiswahili akasikiliza kila kitu

Mwisho mwalimu akaniambia umejieleza vyema Sasa PUT IN ENGLISH hayo yote uliyo nielezea PUT IN ENGLISH

Mzee nikaanza kuwaza Kama DAKIKA KADHAA mwalimu akasema PUT IN ENGLISH.
Nikatoka nje Kama sekunde KADHAA nikarudi nikatema ung'eng'ee mpaka nikajishangaa maana niliflow ngeli wakati sikuwai kukiongea zaidi ya kukiandika..

Pata matatizo nakuhakikishia kingereza utakiongea automatically 🤣😂😅maana ni lugha Kama lugha nyingine tangu WAKATI huo kingereza sijawai kukiogopa kukizungumza..
 
Mie nakumbuka form one Kantalamba,nimefika nikawa kiranja,basi nikashika zamu kuongoza assemble,tumeimba nyimbo zote,ikafika muda wa kuwatawanyisha nikasema "you may disappear" badala "you may disperse" basi ilikuwa gumzo. Ticha akaniita chemba kunielekeza umombo. Ha ha ha
Kuna mmoja alipenda kusema kwa lafudhi ya kisukuma...
AFTER THIS AMALGAMATION form five students should remain asaid.
🤣🤣😂😅
 
Back
Top Bottom