Siku ya kwanza kupigwa ban ulijisikiaje?

Principal Focus

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2013
Posts
925
Reaction score
550
Habari wana JF!

Siku yangu ya kwanza kupigwa ban ama kuwa banned ilikua ni mwaka huu tangu nijiunge toka 2013, basi mwak huu nimetumikia jela ya jamiiforums.

Siku hiyo niliona watu wanafukua makaburi kwenye uzi wangu nikaona mbona wanaongelea kwa tafsiri ya sasa kwa kitu cha 2013, nikaona isiwe tabu ngoja nibadili ujumbe uliopo kwenye thread kisha nikajipeleka mwenyewe kituo kama vile muhalifu anavyojipeleka polisi, ingawa hua naona kwenye movies tu mtuhumiwa anajipeleka mwenyewe basi sie wa kusoma subtitle tuonaona " turn in" ndo na mimi siku hiyo nikajipeleka mwenyewe ku-report thread haina maana.

Basi bila kujua hili wala lie kama masaa mawili kupita sijui hata kesi ilisikilizwa saa ngapi bila mimi kujua nakutana na hukumu tu "umepigwa ban la siku tatu kwa kosa la kuweka thread yenye a.b.c".

Dah hapo nikawaza ndo nakosa kusoma stori za akina Shunie na Money Penny. Siku hizo za kuwa gerezani niliumia sana, jao kuna wengine humu mmeshaona kuwa banned ni kawaida sawa na kula polisi kila siku na kutoka.


Embu sasa tupe uzoefu wako wa kuwa banned siku ya kwanza.Tuseme victims au wahanga wa ban siku ya kwanza ilikuaje na ulijisikiaje?
 
Bado hujawa na akili ww..empty set kabisa
Mimi nahisi wazazi wako waliku- toggle toka jinsia yako sahihi mpaka uliyokuwa nayo, ndio maana umekuja kunitafutika kiki na akili zako za m1-m0. Bora hata ungekuwa base 2 lakini wewe upo base 10... Umetushinda tabia.
 
Nimekula Ban 3 mwaka jana,

Ya kwanza niliipata kwenye uzi wa Le mutuz, baada ya kumquote comment yake nikamtania Mods wakalala mbele na kichwa changu.

Ya pili kwenye jukwaa la Siasa kipindi cha vuguvugu la Lisu alipopigwa risasi, niliipata kwenye uzi wa Chabruma baada ya kutaja jina fulani.

Ya tatu kwenye jukwaa la MMU, nilikuwa najibizana na kapeace, soga zilinoga tukatoka nje ya mada, Mods wakalala mbele na vichwa vyetu mimi na Kapeace.

Ban 2 za mwanzo zilikuwa za siku 5 zote.

Ban ya 3 ilikuwa ya siku 3.

Mwaka huu bado sijapata Ban na najitahidi nisiipate labda iwe kwa bahati mbaya.
 
Mi kuna mtu nilimtukania mamaake bhana bac ckujua ni nn kilitokea ila kila nilipokua naingia humu nyuzi hazifunguki nikahic tu nmelimwa ban. Nilijickia vbaya sana cku ya kwanza nilikua kama mgonjwa
 
Pole sana mkuu kwa kuhunduria jela mara tatu.. Ila hii adhabu hufanya wengi kufungua a/c na kujidai watu wasiojulikana kuja kuattack watu... kapeace wangempa hata adhabu ya kutochangia uzi siku kadhaa ila sio kuwa banned
 
Mi kuna mtu nilimtukania mamaake bhana bac ckujua ni nn kilitokea ila kila nilipokua naingia humu nyuzi hazifunguki nikahic tu nmelimwa ban. Nilijickia vbaya sana cku ya kwanza nilikua kama mgonjwa
Hahaha hukuona sare yao kwenye avatar "banned"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…