Siku ya kwanza kupigwa ban ulijisikiaje?

Mi nilikula ban ya kipuuzi sana. Ilikuwa kule JF doctor zamani kidogo. Jamaa mmoja aliweka uzi akisema kuwa anahisi ana gonjwa la zinaa ila hajui ni gonjwa gani. Akasema dushe lake linatoa usaha na lina madonda na anaogopa kuwa hali ile ikiendelea vile dushe litaweza kudondoka. Basi jamaa wakaanza kuweka picha za magonjwa mbalimbali za madushe yaliyoathiriwa na magonjwa ya zinaa kwa kudhani kuwa kwa vile ilikuwa ni katika muktadha wa medicine ilikuwa sawa. Mi na kimbele mbele changu nikapakua picha kutoka katika medical journal kabisa zikionyesha aina mbalimbali za magonjwa ya zinaa ili jamaa ang'amue ni aina ipi alikuwa nayo. Muda si muda nikaona ile nembo ya kutisha "Banned". Na wote waliokuwa wameweka picha nao wakalimwa ban pia. Siku tatu nzima sikuweza kuingia humu. Mods hawakupi hata onyo aise ukiwatibua ni ban tu kwa kwenda mbele !!!
 
Nimejiunga mwaka 2014 mpaka leo hii sijawahi kupigwa ban
Ungekuwa na post kama zangu na kutopata BAN ingependeza sana, sasa unapost chache jambo ambalo linaonesha huwa huchangii mijadala mara kwa mara na huwezi kupata makosa kwa huo utoro kwenye mijadala.

Hongera kwa kwa kutopata BAN kwa muda mrefu
 
Ungekuwa na post kama zangu na kutopata BAN ingependeza sana, sasa unapost chache jambo ambalo linaonesha huwa huchangii mijadala mara kwa mara na huwezi kupata makosa kwa huo utoro kwenye mijadala.

Hongera kwa kwa kutopata BAN kwa muda mrefu
Mijadala ya jukwaa la siasa nadhani ndiyo inaongoza kwa kupatia watu ban. Huko watu huhemka sana hasa ligi ya mafisi vs manyumbu aka Lumumba vs. Ufipa ikianza. Siku hizi mi nakwenda huko kwa nadra na nikiona moto umeanza kuwaka nasepa zangu kimya kimya..
 
Kweli,
Kama huyo aliyesema ana Ban 15 hadi sasa wakati ID yake ni ya mwaka jana, huwa mkorofi sana kule jukwaa la siasa
 
Ppole sana kuvaa sare la gereza la jf
 
Tangu nijiunge 2009 sijapata ban.
 
Amini usiamini huu mjadala utafungwa kwa MTU kula BANN [emoji23][emoji23][emoji23][emoji188][emoji188][emoji188][emoji188][emoji188]
 
Ndo ilikuwa ban yangu ya kwanza ukweli nilijisikia ovyo sana maana kosa halikustahili adhabu hiyo, baada ya wiki nikapewa ingine tena nikagundua mods ni washenzi tu km wanafiki wengine na wakisoma hapa wanipe ban nyingine na tangu hapo walinimaliza kiherehere humu kwa sasa naingia kwa kunyata then najisepea kimya kimya na sifungui akaunti nyingine km wengine wafanyavyo
 
Pole sana mkuu kwa kuhunduria jela mara tatu.. Ila hii adhabu hufanya wengi kufungua a/c na kujidai watu wasiojulikana kuja kuattack watu... kapeace wangempa hata adhabu ya kutochangia uzi siku kadhaa ila sio kuwa banned
Kuna mods baadhi wanatuibukia pm na maneno ya shombo halafu anakutafutia ban na anakuzawadia kweli hiyo ban ukitoka jela unakuwa konkodi na mvuto wa jf unapungua sana itawaharibia sana hii wasipojirekebisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…