Siku ya Kwanza kwenda kubeba Zege hostel za Magufuli. Moto Uliwaka

Daaah nimecheka kinoma we ni mwamba ulituwakilisha vyema 😂😂😂😂. Kazi za kutumia nguvu sio masihara niliwahi kutembelea mdogo wangu gheto akiwa anafanya field TANESCO, alinisimulia ishu za kuchimba shimo na kuweka nguzo watu wawili... na hapo nikiangalia miguu yake na mikono sikusema kitu ila alivotoka nje chozi lilinitoka.

Hizo kazi vijana wanapambana sana Mungu awajalie.
 
Mimi nilirudishwa nikaambiwa hiyo kazi siwezi ntaacha mwili saa hz natamani nifanye
 
Kwani Huwa hupiti na pikipiki maeneo ya ubungo mpaka gari tu jamaa unafurahisha
 
Hizo mishe nilipiga sana nikiwa ordinary level huko!!ujenzi wa kanisa Fulani hivi kuleee!!nili enjoy sana!yule askofu was very appreciative aiseh!na tulikua hatulipwi just for heaven sake!!

Duuh
Mungu akufungulie Mlango muhimu uliofungwa
 

🤓🤓

Hizi Kazi hutakiwi kuwa muongeaji Sana. Yaani unatakiwa Kuwa mkimya. Niliwaelewa baadhi ya wakongwe wa mishe hizo
 
🤣🤣🤣Kuna mwenzako humu alileta stori ya zege na akaambiwa hapa maji utaita mma na kweli alikiri maji aliyaita mma ,tena sio mara moja.Picha linaanza waliambiwa washushe mifuko ilikuwa kitu ka buku au mia sita ,sikumbuki vizuri.
Kikawaida Gari ya mizigo inabeba tani 30,
Mfuko wa saruji Una kilo 50.

Tani 30 ni sawa na kilo 30000 kwahiyo unagawanya
Kwani Huwa hupiti na pikipiki maeneo ya ubungo mpaka gari tu jamaa unafurahisha
Sasa kama ni daladala aseme ni pikipiki 🤣
 
Dah Nimecheka Saana
 
Aiseee,acha kabisa hzo mishe,kwa sisi tuliopitia kushika kalamu muda mrefu huwez toboa
Basi babu siku moja nikapewa tipa zile za blue, Za kizamani nikasema, kweli mimi ni "dere" mzuri navunja mihogo kama Sina akili(mihogo Yani gear leaver) 😝🤣

Nikaambiwa Aya itoe kwenye mteremko ipandishe ukasimamie mlimani ubalance clutch bila brake

, baba nikaweka gear no.1 ,ile kufika pale mlimani kubalance nusu clutch, chuma ilirudi nyuma😝🤣nilipiga yowe oya wakubwa🤣Njooni mnitoe

Sita sahau hiyo siku alafu brake zilikuwa chache
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…