Siku ya Kwanza kwenda kubeba Zege hostel za Magufuli. Moto Uliwaka

Siku ya Kwanza kwenda kubeba Zege hostel za Magufuli. Moto Uliwaka

Kwamba wasababishi washaanza kujitokeza
Hahahahaha!! ila Mimi mwenyewe wakati namaliza Advance sikuenda jeshini na nilikaa mwaka mmoja kitaa , baada ya kukaa stationery mahali na kujifunza computer skills na kuhudumia biashara mbalimbali za pale nikaamua nirudi nyumbani nifungue twisheni uchwara ya kuzugia niwafundishe madogo wa mtaani kusudi nipate muda wa kutoka ,kutembea na kufanya yangu mengine ya msingi maana pale palikuwa pananibana halafu kwa ndugu tu aliniita ili nijifunze na nimsaidie tu.

Baada ya muda nikaona nibadilishe nitoke niende mbali nikapige vibarua vya UJENZI , kwa hakika niliyatimba kisawasawa tokea hapo nikawa nathamini sana pesa maana nimeshuhudia jinsi tulivyokuwa tunapigika kiugumu mpaka kuingiza pesa japo nilipata tabu sana siku za Mwanzo Kisha nikazoea nikapiga kwa kwa takribani mwezi mmoja na kitu.
 
😂😂😂
 
Hizo kazi ni mazoea tu na usipambane kuonesha umwamba wa kutumia nguvu zako nyingi kwa sifa lazima kesho usiibuke site.

Unazingonga mdogo mdogo kiufundi halafu ili mwili uzoee kesho tena unaibuka site mdogo mdogo mpaka mwili unazoea
 
Tatizo langu Nina sifa za kijinga. Nilitaka nionyeshe umwamba kwa madogo
 
Hapana Mkuu! Hiyo Kazi ni Kiboko ya mabishoo na wavivu
Kazi za kupinda kiuno kuanzia 12:00 mpaka usiku haah hatari ukiwa mrembo lazima ukimbie.

Machalii wengi waliokuwa wanakuja site walikuwa wanatema madeal wanapita mbele wanasema kazi ngumu😀
 
nakumbuka nilishawah kubeba zege nikiwa advance kipind chalikizo kwa hali niliyopitia ilibid nichukue mablanket nivilingite kama gogo niweke katikat ya kiuno nikilala ili mgongo unyooke
 
Tatizo langu Nina sifa za kijinga. Nilitaka nionyeshe umwamba kwa madogo
Haah hizo kazi ni mwili tu kuzoea na sio sifa za matumizi ya nguvu nyingi kama watu wengi wanavyo dhani na ndipo wanapofeli hapo.

Wanakuja na mbwembwe wakipiga chepe kadhaa wanatema ndoano.

Unaweza kuta site janja ana mwili mdogo tu ila anazikimbiza hizo kazi mbaya mbovu sasa wewe ukimpimia kwa mwili wake na ukicheki body lako utahisi na mimi naweza na hawezi nishinda huyu kumbe mwenzako mzoefu unaingia na sifa zako karai/ndoo kadhaa jasho jingi, kiuno kinauma, mabega,mgongo unaamua kutema dili na kukimbia😀
 
Iyo mbanga naijua. Pia Kuna ile ya kufyatua tofali za block 6×9 inches zinazotengenezwa kwa machine ya umeme. Ni mchanganyiko wa dust, morum na cement inatokea tofali nzito sana, ikiwa mbichi ni wastani wa 50kg kwa tofali moja. Kwa machalii wa Arusha USA- river na Majibya Chai wanaelewa, show ni kwere
 
Kuna jamaa yangu anaitwa sheby

Aliwahi nisumulia story kama hii yeye alikuwa mambo safi tu nyumbani sema

Alizinguana na family yake plus dada zake kukawa kuna conflicts

Hivi sheby anasema aliona ajitoe ki home kwenda kutafuta mchongo

Akapa mchongo kama wako aiseh jinsi ulivyo simulia ni kama yeye 😂😂😂🙃🙏

Nimecheka sana yeye anasema jioni alipopewa hiyo 15 akasema

Haki sitorudi tena hapa

Kesho yake ikabidi kujirudi kwa sister zake hapo kwao

sasa ikabidi Awaambie kuhusu huo mkasa

Anasema nyumbani kwao hakuwahi kuona wakicheka kwa furaha kama hiyo siku 😂😂😂😂
 
😃😃😃Zege sio mchezo.
 
😂😂
 
SIKU YA KWANZA KWENDA KUBEBA ZEGE HOSTEL ZA MAGUFULI. MOTO ULIWAKA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli

Nipo zangu likizo wakati nasoma, basi Taikon nikaenda Tandale kwa Mshikaji wangu, Classmate. Ilikuwa jumapili hivi, mfukoni Niko na pesa za Serikali, Bumu zinanisumbua.

Baada ya kuonana naye tukatoka kwenda kujivinjari maeneo ya beach zilizopo Kigamboni. Serikali ilishanipa pesa kuhusu matumizi ilikuwa juu yangu. Tukiwa huko Kigamboni kwenye Moja ya Beach za kulipia. Huku macho yetu yakiwa kodokodo kwa watoto wakali waliokuwa wakikata Maji. Hakika tuli-enjoy Sana.

Mshikaji akaniambia itabidi tuwahi kurudi home kwa Sababu Kesho, jumatatu anaratiba ya kwenda kazini maeneo ya Udsm kwenye Ujenzi wa hostel ambazo Leo hii zinaitwa Magufuli Hostel.
Nikamuuliza kwa siku wanalipa bei gani akaniambia ni 25,000 kwa wanyanyua zege na mafundi Chuma.

Kusikia elfu 25 Roho ikanitoka,kumbe mnalipwa pesa nyingi Sana,nikasema.

Hapo akilini nikipiga hesabu zangu kuwa nikifanya siku Tatu elfu 75, nikifanya siku 20 napata Laki mbili na hamsini (250,000/=) mamaaaaa! 250,000 siku kumi........!!

Haaaa! Kwa kweli nilivutiwa na hiyo habari hivyo nikamwambia Mshikaji kuwa kama kuna Nafasi tunaweza kwenda wote. Akaniambia Nafasi ipo.

Tukarudi zetu, yeye akaenda Tandale kwake na Mimi nikarudi Sinza Kwaremi nilipokuwa naishi.

Nakumbuka siku hiyo Taikon Wala sikutaka kufungulia Luninga Wala Muziki, sikutaka kuingia mtandaoni.
Nilikuwa zangu nimechukua Calculator na kidaftari nikifanya mahesabu ya jinsi pesa nitakazozipata kutokana na kubeba Zege.

Likizo ilikuwa ya miezi miwili kama mjuavyo likizo za chuoni. Hivyo nilikuwa na siku zisizopungua siku 60 za kunyanyua Zege.

Mahesabu yakaanza,
Siku 60 × 25,000/=. 1,500,000/=
Tobaaaa!

Kwamba Mpaka Chuo kinafunguliwa nitakuwa na 1.5M kibindoni. Haaaah! Sitaki kuamini kama kweli kuna pesa zilikuwa zinanipita hivihivi kizembe. Basi nikawa najilaumu Sana kwa kuzembea.

Hiyo pesa nikasema nitanunulia pikipiki nitaongezea tuu kidogo na pesa ya Bumu niliyokuwa nayo.
Sasa nikaanza mahesabu ya jinsi pikipiki itakavyoniingizia pesa.

Kwa siku nitaingiza elfu 10. Kwa mwezi Laki Tatu. Jumlisha Bumu haaaah Mimi sio mwenzenu tayari nimeipata channel. Kwamba ningekuwa mwanachuo mwenye kipato cha uhakika.

Mahesabu yangu yalinionyesha kwa mwezi nitakuwa na kipato cha Akiba kama Laki nne hivi. Kwa mwaka ningekuwa na 4.8M. haaaah! Kwa kherini makapuku!

Kumbuka hizo ni imagination tuu na mahesabu kabla ya tukio. Kuangalia Sana ilikuwa saa tano inaenda saa sita.

Nikasema Acha nikalale ili asubuhi nimke nikiwa na nguvu. Panda kitandani tafuta usingizi.

Sasa mawazo yakawa yananipitia jinsi wakati nasoma watu na jamii ilivyokuwa inanichukulia. Wengi waliniambia Nisome Sana kwani Kazi za nguvu Mimi sitawezana nazo. Oooh! Wewe ni Bishooo! Ooh! Wewe ni shalobaro Kazi za nguvu zinawatu wake, watu Kazi yaani nguvu Kazi ya taifa na sio wewe(yaani Mimi)
Nilikuwa nakumbuka Maneno hayo.

Nikasema kwa sauti ya chini, huu ni wakati sasa wa kuonyesha kuwa nimekua Mkubwa sasa, nami ni mwanaume wa shoka. Wazazi wangu wakisikia hii wataniona shujaa. Na watajivunia Sana.

Huuuuu! Nimekua bhana!
Nikalala.

Asubuhi ikafika, hao Mpaka Site.

Tukaagana na mshikaji wangu yeye alikuwa idara ya ufundi chuma akaenda upande mwingine Mimi nilikuwa idara ya kubeba Zege.

Kazi ikaanza, ni asubuhi hapo Jua bado halijaanza,

Beba ndoo mbili zile ndogo zenye Uji wa Zege. Pandisha ghorofa ya pili.
Mwanzoni niliona sio Kazi nzito Sana kama nilivyokuwa naihofia.

Kilichonitia moyo zaidi ni kuona kuna vijana wawili wadogo zaidi kiumri na Kimwili waliokuwa pale nao wakipiga Mzigo.

Imefika saa mbili hivi kajua kapo juujuu mwili umechemka balaa. Kazi inafanyika nakuambia ungeniona Muda huo ungesema kweli huyu Kijana ni nguvu Kazi ya taifa. Mtu kazikazi.

Jasho lanitoka, mapigo ya moyo yanapiga, damu inakimbia balaa. Mimi sijali.

Nikawa nasema kimoyomoyo
" Robert huo ndio uanaume"
Napandisha ngazi mbili nasema,
" Mwanaume kazini"
Nameza mate kisha napanda ngazi nyingine alafu nasema
" Hapa Kazi sicheki na Kima"

Wale vijana nao sijui walikuwa wanashindana na Mimi wakawa wanatembea harakaharaka kubeba Zege na kwenda ghorofani kumwaga na kushuka chapuchapu!

Msinitanie nyie! Hamnijue eeeh!
Nikasema kimoyomoyo kama mjuavyo Taikon Master ninasifa za kijinga na sitaki kushindwa kienyejienyeji. Dadeki!

Huyo nikaanza kukimbia na zile ndoo ndogo mbili za Zege kama kiberenge, rapu!rapu! Rapu! Rapu! Upesiupesi nikisonga na kupanda ngazi na kumwaga Kule ghorofani na kushuka harakaharaka kama nipo Depo.

Nikashuka upesiupesi tena nikawakuta wale vijana ndio wanamaliziwa kuwekewa Zege, nikafika pale wakawa wananitazama nami Wala sikujali nikawaona wakikubali kuwa Mimi sio mgeni WA Kazi zile. Na Mimi lengo langu ndio lilikuwa lile.

Nina Experience Mimi kumbe ndio siku ya Kwanza hiyo.

Wakaondoka, kisha nikabeba tena upesiupesi kuwawahi kabla hawajafika ghorofani. Mara sijui namna gani pale nikajikwaa, chini na ndoo huko ilikuwa napanda kwenye ngazi. Hapakuwa na mtu. Dadeki! Aibu hii! Nikarudi chini kinyemela nikiwa na ndoo nusu hivi.

Nikajibanza sehemu Wale madogo wakapita wakashangaa kuona Zege limemwagika hawajui nani kamwaga. Walipopita akapanda mtu mwingine kisha akashuka mtu mwingine nami ndio nikajitokeza kinyemela nikarudi kuchukua Mzigo. Nakutana na wale madogo Mmoja kaweka ndoo kichwani alafu ndoo mbili kabeba mikononi. Mmmh! Nikaropoka, kuna mtu kamwaga Zege kule kwenye ngazi alafu wewe unajifanya kubeba kichwani.

Wale wakoroga Zege wakauliza Nani kamwaga Zege huko. Basi likazuka zogo Mimi Kimya.
Saa nne hiyo.

Sasa kufika Sana tano Jua limeshachanganya, mwili umepata moto Mpaka unataka kuwaka, Koo limekauka, tumbo linanjaa, kifupi naona na knockout. Watu hawazungumzii mambo ya breakfast. Mmmh!

Pumzi inakata!

Wale madogo ndio Kwanza kumekucha kwao ndio asubuhi. *****!
Hawa wajinga wataniua hawa!

Mikono inauma!
Viganja kama vinataka kukatika!
Vidole vya mikononi vinauma!
Mabega yanauma!
Kudadadeki!

Watu hawataki ufafanuzi Wala maelezo. Hapa Kazi tuu!
Hakuna cha mambo ya unajua sijui oooh! Reference sijui nini wala nini!! Fasihi zako Peleka huko! Huku ni nguvu Kazi ya taifa tuu!

Saa sita unusu hiyo! Masaa nayo yameganda na Jua linachoma balaa.

Midomo imepauka, macho yameshaanza kuwa mekundu hakika ningedhaniwa ni mchawi asilani Kule kwenu shinyanga.

'" Kwani nikiacha sasa hivi hawatanipa angalau Nusu ya Ile Pesa"
Ninawaza huku nikiwa na jikongoja Dunia nimeibeba begani.

"Mimi hata walinipa elfu kumi tuu inatosha, kumaliza Mpaka saa kumi na mbili sio kweli"
Saa Saba hiyo.

Mara mwanaume Mmoja mwenye lafudhi ya kisukuma ambaye alikuwa akiongeaongea ambaye baadaye nilijulishwa ndiye Injinia Msimamizi katika Moja ya Majengo tunayoyajenga akatuambia tufanye chapuchapu kwenda Kula kisha tuwahi kurudi. Tulipewa Nusu saa tuu.

Huuu! Mshikaji akanikuta nimechoka balaa. Alinicheka Sana.
Tunamaliza Kula. Kazi ikaendelea

Mpaka inafika jioni Zege linaisha aiseeh! Moto uliniwakia.

Tukamaliza tukaambiwa Kesho tuwahi kuendelea na kipande kingine. Kuhusu pesa nikajulishwa Mtoa pesa hayupo ila Kesho tutalipwa. Bwaah! Kesho tena.
Wakati Mimi nilishaapa sitoweza kurudi tena pale hata kwa risasi.

Nikarudi nyumbani, nimechoka balaa. Nikaoga,
Nikazima TV
Nikazima Simu
Nikazima umeme main Switch.
Yaani sikutaka usumbufu wa aina yoyote. Nilitaka niwe kama nipo kaburini. Tuli! Kimya!

Nikalala zangu.
Nakumbuka siku hiyo nililala kama nimekufa. Fofofo ndio Ile Bwana.

Asubuhi naamka ni kama Mgonjwa aliyetoka kwenye Koma. Sikumbuki chochote. Mwili mzito

Nikipiga miayo mbavu zinauma.
Najaribu kunyanyua Mikono na miguu nashindwa.

"Mmmh! Niko wapi?"
Nikawa nageuza macho huku na huku kama mjusi wa ukutani kwani nilishindwa kugeuza shingo ambayo ilikuwa inauma na imekakamaa.
Hiyo hela Yao wabaki nayo.

Mipango ya kununua pikipiki ikafa palepale. Sijui 25 time ngapi kwendraa. Nyoko!

Moto uliniwakia!
Acha nipumzike tuu.
Nikipita na gari maeneo ya ubungo Mawasiliano nikiziona zile hosteli nabaki nacheka tuu.

Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam
Hahahahahahahaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]

Mbona zege cha mtoto niliwahi kufanya kazi bandarini pale kigoma ni hatari unashuka kwenye meli kule chini wanaita "ndelepoo" halafu winchi linashusha mizigo mnakua mnaipanga mamaeeee... Ungekufa
 
Zege linatisha.. Nishawahi kuona kibarua anaiba nguo zake alizovua kabla ya kuanza kazi ya kubeba zege... Aliziibaa na posho akasamehe... Akaingia mitini..
 
Iyo mbanga naijua. Pia Kuna ile ya kufyatua tofali za block 6×9 inches zinazotengenezwa kwa machine ya umeme. Ni mchanganyiko wa dust, morum na cement inatokea tofali nzito sana, ikiwa mbichi ni wastani wa 50kg kwa tofali moja. Kwa machalii wa Arusha USA- river na Majibya Chai wanaelewa, show ni kwere
Sasa hivi wanabeba na vigari kama vitoroli very easy
 
Back
Top Bottom