Siku ya Kwanza kwenda kubeba Zege hostel za Magufuli. Moto Uliwaka

Kwamba wasababishi washaanza kujitokeza
Hahahahaha!! ila Mimi mwenyewe wakati namaliza Advance sikuenda jeshini na nilikaa mwaka mmoja kitaa , baada ya kukaa stationery mahali na kujifunza computer skills na kuhudumia biashara mbalimbali za pale nikaamua nirudi nyumbani nifungue twisheni uchwara ya kuzugia niwafundishe madogo wa mtaani kusudi nipate muda wa kutoka ,kutembea na kufanya yangu mengine ya msingi maana pale palikuwa pananibana halafu kwa ndugu tu aliniita ili nijifunze na nimsaidie tu.

Baada ya muda nikaona nibadilishe nitoke niende mbali nikapige vibarua vya UJENZI , kwa hakika niliyatimba kisawasawa tokea hapo nikawa nathamini sana pesa maana nimeshuhudia jinsi tulivyokuwa tunapigika kiugumu mpaka kuingiza pesa japo nilipata tabu sana siku za Mwanzo Kisha nikazoea nikapiga kwa kwa takribani mwezi mmoja na kitu.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Mbona kazi ya kawaida hiyo mkuu
 
Hizo kazi ni mazoea tu na usipambane kuonesha umwamba wa kutumia nguvu zako nyingi kwa sifa lazima kesho usiibuke site.

Unazingonga mdogo mdogo kiufundi halafu ili mwili uzoee kesho tena unaibuka site mdogo mdogo mpaka mwili unazoea
 
Hizo kazi ni mazoea tu na usipambane kuonesha umwamba wa kutumia nguvu zako nyingi kwa sifa lazima kesho usiibuke site.

Unazingonga mdogo mdogo kiufundi halafu ili mwili uzoee kesho tena unaibuka site mdogo mdogo mpaka mwili unazoea

Tatizo langu Nina sifa za kijinga. Nilitaka nionyeshe umwamba kwa madogo
 
Hapana Mkuu! Hiyo Kazi ni Kiboko ya mabishoo na wavivu
Kazi za kupinda kiuno kuanzia 12:00 mpaka usiku haah hatari ukiwa mrembo lazima ukimbie.

Machalii wengi waliokuwa wanakuja site walikuwa wanatema madeal wanapita mbele wanasema kazi ngumuπŸ˜€
 
nakumbuka nilishawah kubeba zege nikiwa advance kipind chalikizo kwa hali niliyopitia ilibid nichukue mablanket nivilingite kama gogo niweke katikat ya kiuno nikilala ili mgongo unyooke
 
Tatizo langu Nina sifa za kijinga. Nilitaka nionyeshe umwamba kwa madogo
Haah hizo kazi ni mwili tu kuzoea na sio sifa za matumizi ya nguvu nyingi kama watu wengi wanavyo dhani na ndipo wanapofeli hapo.

Wanakuja na mbwembwe wakipiga chepe kadhaa wanatema ndoano.

Unaweza kuta site janja ana mwili mdogo tu ila anazikimbiza hizo kazi mbaya mbovu sasa wewe ukimpimia kwa mwili wake na ukicheki body lako utahisi na mimi naweza na hawezi nishinda huyu kumbe mwenzako mzoefu unaingia na sifa zako karai/ndoo kadhaa jasho jingi, kiuno kinauma, mabega,mgongo unaamua kutema dili na kukimbiaπŸ˜€
 
Iyo mbanga naijua. Pia Kuna ile ya kufyatua tofali za block 6Γ—9 inches zinazotengenezwa kwa machine ya umeme. Ni mchanganyiko wa dust, morum na cement inatokea tofali nzito sana, ikiwa mbichi ni wastani wa 50kg kwa tofali moja. Kwa machalii wa Arusha USA- river na Majibya Chai wanaelewa, show ni kwere
 
Kuna jamaa yangu anaitwa sheby

Aliwahi nisumulia story kama hii yeye alikuwa mambo safi tu nyumbani sema

Alizinguana na family yake plus dada zake kukawa kuna conflicts

Hivi sheby anasema aliona ajitoe ki home kwenda kutafuta mchongo

Akapa mchongo kama wako aiseh jinsi ulivyo simulia ni kama yeye πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ™ƒπŸ™

Nimecheka sana yeye anasema jioni alipopewa hiyo 15 akasema

Haki sitorudi tena hapa

Kesho yake ikabidi kujirudi kwa sister zake hapo kwao

sasa ikabidi Awaambie kuhusu huo mkasa

Anasema nyumbani kwao hakuwahi kuona wakicheka kwa furaha kama hiyo siku πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒZege sio mchezo.
 

πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hahahahahahahaha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]

Mbona zege cha mtoto niliwahi kufanya kazi bandarini pale kigoma ni hatari unashuka kwenye meli kule chini wanaita "ndelepoo" halafu winchi linashusha mizigo mnakua mnaipanga mamaeeee... Ungekufa
 
Zege linatisha.. Nishawahi kuona kibarua anaiba nguo zake alizovua kabla ya kuanza kazi ya kubeba zege... Aliziibaa na posho akasamehe... Akaingia mitini..
 
Sasa hivi wanabeba na vigari kama vitoroli very easy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…