Siku ya kwanza uliposafiri

Tupo wengi mdogo.

Miss you too mdogo. Nipo Dada yako mambo tu zinakuwa mingi saa ingine. Natumai uko mzima?

Mimi sikulala kabisa nilikuwa naelekea DaresSalaam yaani nililala saa kumi na mbili jioni saa mbili nimeamka usiku na sikulala kabisa mpaka alfajiri. Alafu nilijua DaresSalaam udongo ni tofauti na kwetu kumbe yaani niliumia kuona watu maskini kuliko hata nilikotoka .

Alafu nilipoona gari linakimbia oh miti inarudi nyuma nikaanza kutapika balaaa.
 
Hahahahaaa. Lol

Hivyo Mkuu ulijua Daslam tuna udongo wetu? πŸ˜‚
 
Umenikumbusha mbali mie kipindi ndio nakuja Daslam nilipata sana shida na zile taa za pembezoni mwa barabara kwa jinsi zinavyowaka mana nilikotoka huko hazikuwepo.

Niliduwaa mpaka leo sijuagi lile basi ndo lilipitaga wapi mana nilishukaga Ofisini πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…