Siku ya Mashoto Duniani: Wana JF wenzangu tunaotumia mkono wa kushoto tukutane hapa

Happy International left handers day
Happy birthday to you Fareed Kubanda aka Fid Q
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
nilipata sana shida kutumia mkono wa kulia hasa wakati wa kula chakula nilikuwa sishibi mpka nitumie mkono wa kushoto,
 
Kuna mwalimu wakati nipo shule ya msingi alinisumbua sana kunitaka nitumie kulia lakin jitihada zake ziligonga mwamba na nilijikuta namchukia kweli kweli, kila kitu nafanya kwa mkono wa kushoto isipokuwa kula na kusalimiana na mtu hapo ndipo nakoshangaa maajabu ya mungu
 
Asante kwa kutukumbusha na kutoa shule. Mimi ni malia lakini nina mtoto mashoto. Ninamjulisha mara kwa mara baadhi ya mambo uliyoyataja hapa. Anajikubali na ameshajua amtazamo wa jamii juu ya watu kama yeye.

Jambo ambalo bado wanapata changamoto ni jamii kutowatambua hasa katika vitu vinavyotengenezwa na binadamu. Vingi hutengenezwa kwa mtazamo wa MALIA na hivyo wao kujikuta wakipata changamoto. Kwa mfano uwekaji wa vitasa na makomeo. Kuna haja ya kuwakumbuka kundi hili la binadamu. Tujitahidi kutoa elimu jizi kwenye familia ili watoto wakue wakifahamu uwepo wa watu hawa na ni binadamu wa kawaida kama wengine ili kuepuka unyanyapaa.

Sema mimi ninakosa raha, hivi hatuwezi kuita jina lingine zaidi ya mashoto? Unajua hili tumekuwa tunalitumia kwa mtazamo hasi. Ndiyo maana unaona hatuna MALIA wala MALIAMASHOTO (wenye kuchanganya yote) bali tuna MASHOTO.

Shukrani sana mtoa mada
 
I may be left-handed, but I am always right.

#Happy left-handers day.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…