Cute Wife
Platinum Member
- Nov 17, 2023
- 3,054
- 8,449
Siku ya Mitandao ya Kijamii Duniani inayoadhimisha Juni 30 ya kila mwaka, ilianzishwa na mtandao wa Mashable mnamo mwaka 2010, adhimisho hili la kimataifa linaangazia mapinduzi makubwa yaliyofanywa na mitandao ya kidijitali kwenye mifumo ya mawasiliano, biashara, na utamaduni.
Taarifa Muhimu (2026):
Kulingana na Data Reportal;
Ingawa intaneti imeendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania (ifikapo mwisho wa mwaka 2025, ufuatiliaji ulionyesha kufikia usajili wa intaneti milioni 58.1), ripoti (Wasilisho la Pamoja la Wadau Kuhusu Mapitio ya Kipindi cha Nne cha Universal Periodic Review (UPR) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 2026) inaeleza kuwa nafasi ya kiraia na uhuru wa kidijitali vimeendelea kushuka kwa kasi. Serikali imekuwa ikitumia sheria na kanuni mbalimbali kukandamiza sauti zinazopingana nayo au zinazoikosoa.
Kwa jinsi hali ya kisiasa inavyoendelea nchini inaonyesha hali uhuru wa mitandao ya kijamii, majukwaa na uhuru wa wananchi kujieleza kwenye majukwaa haya kwa ujumla kuendelea kuporomoka hasa kwa kuwa serikali inaendelea kuminya vyombo hivi na sheria kandamizi kuendelea kuwepo bila kufanyiwa maboresho, pamoja na presha kulingana na hali ya kisiasa nchini.
Hivi sasa kuna taarifa za wananchi kufanya Maandamano ya Amani nchi nzima Julai 7, siku ambayo ni Maadhimisho ya Kitaifa ya Biashara 77, hili pia linaongeza presha kwa serikali kuzidi kuminya mitandao hii ambayo imekuwa inatumika kwa kiasi kikubwa na wananchi kuwasilisha kero zao na kuikosoa serikali pale wanapoona mambo yanaenda ndivyo sivyo.
Taarifa Muhimu (2026):
- Takriban watu bilioni 4.95 wanatumia mitandao ya kijamii kikamilifu duniani kote.
- Wastani wa mtumiaji mmoja duniani anatumia takriban saa 2 na dakika 27 kwenye mitandao ya kijamii kila siku.
- Kutokana na kukua kwa mitandao ya kidijitali, matukio ya utapeli yameongezeka kwa kasi kubwa, huku mitandao ya kijamii sasa ikiipita barua pepe (email) kama njia kuu inayotumiwa zaidi kufanya utapeli wa mtandaoni.
- Tanzania ina jumla ya usajili wa intaneti (internet subscriptions) milioni 58.9 (hadi kufikia Machi 2026), ambayo ni sawa na zaidi ya watumiaji binafsi hai (active individual users) milioni 30 wa intaneti.
Kulingana na Data Reportal;
- Facebook: Ndio mtandao unaoongoza ukiwa na watumiaji milioni 7.95 (sawa na 11.2% ya watu wote). Uliongeza watumiaji milioni 2.05 (+34.7%) kwa mwaka huo.
- Instagram: Inashika nafasi ya pili ikiwa na watumiaji milioni 4.10 (sawa na 5.8% ya idadi ya watu wote). Ilikuwa kwa watumiaji laki 6 (600,000) (+17.1%).
- LinkedIn: Ina wanachama (members) milioni 1.70 (sawa na 2.4% ya watu wote). Ilikua kwa wanachama laki tatu (300,000) (+21.4%). Kumbuka: LinkedIn inahesabu akaunti zilizosajiliwa, sio watumiaji hai wa kila mwezi.
- Messenger: Inatumiwa na watu milioni 1.40 (sawa na 2.0% ya idadi ya watu wote). Ilikua kwa watumiaji laki moja (100,00) (+7.7%).
- Reddit: Ina watumiaji laki moja na kumi na moja (111,000) (sawa na 0.2%). Ingawa idadi yake ni ndogo, ilionyesha ukuaji mkubwa wa asilimia +309% (ongezeko la watumiaji elfu 83.6).
- X (zamani Twitter): Inashika nafasi ya mwisho ikiwa na watumiaji elfu 90 (ikiwa ni sawa na 0.1% ya idadi ya watu wote).
Ingawa intaneti imeendelea kukua kwa kasi nchini Tanzania (ifikapo mwisho wa mwaka 2025, ufuatiliaji ulionyesha kufikia usajili wa intaneti milioni 58.1), ripoti (Wasilisho la Pamoja la Wadau Kuhusu Mapitio ya Kipindi cha Nne cha Universal Periodic Review (UPR) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 2026) inaeleza kuwa nafasi ya kiraia na uhuru wa kidijitali vimeendelea kushuka kwa kasi. Serikali imekuwa ikitumia sheria na kanuni mbalimbali kukandamiza sauti zinazopingana nayo au zinazoikosoa.
Changamoto Kuu Kwenye Mitandao ya Kijamii & Uhuru wa Kujieleza
- Sheria na Faini Kandamizi (EPOCA Regulations): Kanuni za maudhui ya mtandaoni (Online Content Regulations kama zilivyorekebishwa 2022 na 2025) zinamlazimu kila mtoa huduma wa mtandao kuwa na leseni kutoka TCRA. Kutofanya hivyo kunasababisha kifungo cha hadi miezi 12 au faini ya angalau Shilingi Milioni 5.
- Kufungiwa kwa JamiiForums na Mifumo Mingine (tukio la karibu kabisa kufungiwa kwa Jambo TV April 2026): Mnamo Septemba 2025, TCRA ilisimamisha leseni ya JamiiForums kwa siku 90, lakini jukwaa hilo liliendelea kuzuiwa (blocked) kwa zaidi ya miezi sita hadi kufikia mapema mwezi Juni 2026. Hii ilitafsiriwa kama shinikizo kwa jukwaa kubwa la kutoa taarifa za siri (whistleblowing) nchini.
- Kuzimwa kwa Intaneti Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2025: Wakati wa kipindi cha uchaguzi mkuu (kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3, 2025), serikali ilizima mtandao (internet shutdown) ya siku tano nchi nzima. Hii ilisababisha kukosekana kwa taarifa (information blackout) kwa kukata kabisa mitandao kama X (Twitter), TikTok Live, na Instagram Live.
- Udhibiti wa Mitandao kwa kutumia VPN: Baada ya kuzuiliwa kwa App ya Clubhouse mnamo 2023 na wananchi kuanza kutumia VPN, TCRA ilipiga marufuku matumizi ya VPN ambazo hazijasajiliwa, hatua inayokiuka haki ya faragha na uhuru wa kupata habari.
- Kukamatwa kwa Wanaharakati na Waandishi: Wanaharakati mbalimbali wamekumbana na mashtaka makubwa; kwa mfano, mnamo Oktoba 2025 mwanaharakati Mika Chavala alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini (treason) baada ya kuweka video Instagram akishiriki maandamano. Pia, mwaka 2024 kulirekodiwa matukio 10 ya ukamataji na unyanyasaji wa waandishi wa habari (ikiwemo kutoka Jambo TV na Mwananchi).