Mawazo ya kuwepo kwa siku ya kimataifa ya vijana yalitolewa mnamo mwaka 1991 na vijana waliokusanyika mjini Vienna nchini Austria kwa ajili ya kipindi cha kwanza cha jukwaa la dunia la vijana la mfumo wa umoja wa mataifa.
Kwa mara ya kwanza, Umoja wa Mataifa ulisherehekea mwaka wa kimataifa wa vijana mnamo mwaka 1985 ambapo mwaka 1999, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha tarehe 12/Agosti kuwa siku ya kimataifa ya vijana ambayo ilisherehekewa kwa marea ya kwanza mwaka 2000.
Siku ya vijana duniani husherehekewa ikiwa na lengo la kutambua na kusherehekea juhudi za vijana katika masuala mbalimbali kama wadau wa jamii ya kimataifa. Siku hii pia hutumika kuwahamasisha vijana kushiriki katika masuala mbalimbali ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao.
Kama hilo halitoshi, siku hiyo pia hutumika kwa ajili ya kutoa uelewa kwa jamii na kupaza sauti kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazoiwagusa vijana ikiwemo ajira, afya, elimu na ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za uongozi.
Kila mwaka huwa kuna kauli mbiu tofauti tofauti kwa ajili ya kusherehekea siku hii ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni "Mshikamano wa vizazi: Kuunda Ulimwengu kwa Vizazi zote" ikiwa na lengo la kuhamasisha na kuimarisha ushiriki wa vizazi vyote katika kufikia malengo endelevu yaliyowekwa yaliyowekwa na umoja wa mataifa mwaka 2015.