Wachina wanasema, “maneno matupu yanaidhuru nchi, kazi kwa bidii inastawisha nchi.” Lakini je, bidii ni nini? Cha muhimu ni kufanya kazi moja baada ya nyingine. Miaka michache iliyopita, katika mazungumzo na wajumbe wa wafanyakazi bora wa kitaifa, rais Xi Jinping wa China naye alinukuu msemo mmoja uliosemwa na Qian Decang kutoka enzi ya Qing, ukisema “hakuna kitu kigumu wakati bidii ipo". Ndani ya miongo kadhaa tu, China imeweka miujiza mingi mbalimbali kwa kutimiza ndoto za kusafiri anga za juu, kufanya michezo ya Olimpiki, kutua mwezini, hayo yote ni matokeo ya kazi ngumu ya wafanyakazi.
China na nchi za Afrika hivi leo zote zinakabiliwa na kazi kubwa za kutafuta maendeleo na watu pia wanatarajia kutimiza ndoto mbalimbali binafsi. Hata hivyo, kadiri hali inavyokuwa ngumu, ndivyo inavyohitajika zaidi kutegemea bidii, kazi ya uadilifu, na ubunifu ili kufikia ndoto ya maendeleo ya nchi na watu binafsi.