Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hizo picha mbili hapo chini zote zimepigwa siku za mwanzo kabisa za kuundwa kwa TANU na kuanza kwa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Nimechagua picha hizi mbili ili kuonyesha haiba ya wanawake wapigania uhuru wa Tanganyika.
Wanasema picha inazungumza maneno 1000 na pia jicho la camera linaona kile ambacho jicho la binadamu limeona.
Hakuna tofauti.
Picha hii hapo juu imepigwa Mnazi Mmoja kati ya mwaka wa 1954 na 1955 na ni katika picha za zamani za mikutano ya TANU Viwanja Vya Mnazi Mmoja.
Ukiangalia vizuri utaona na huo Mnazi Mmoja ulitoa jina la viwanja hivi.
Angalia upande wa kushoto wa picha hii utaona kuna sehemu imetengwa na ina rangi nyeusi.
Huo weusi ni mabaibui ambayo wanawake waliokuwa wanakuja katika mikutano ya TANU wanavaa kujisitiri.
Lakini wangapi leo wanajua haya mabaibui na wavaaji wake walikuwa wanonekanaje?
Nakuwekea hapo chini picha ya pili uone:
Kulia ni Chiku bint Said Kisusa, Bibi Titi Mohamed (jina halikupatikana), Julius Nyerere, Lucy Lameck na Tatu bint Mzee wakimsindikiza Nyerere Uwanja wa Ndege Dar es Salaam safari ya kwanza UNO 1955.