Siku ya Wanawake Duniani: Who Are The Top Ten Richest Women In Tanzania?!

Siku ya Wanawake Duniani: Who Are The Top Ten Richest Women In Tanzania?!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye akili, uwezo, na utajiri. Je wanawake kumi ambao ni matajiri wakubwa Tanzania ni kina nani, utajiri wao nini, na umetokana na nini?.Sehemu ya kwanza kupiga hodi ni kwenye jarida la forbers!.

Huku sikukuta hata jina moja la mwanamke yoyote tajiri kutoka Tanzania!, hii maana yake, hatuna mwanamke yoyote tajiri mwenye viwango vya utajiri wa kimataifa, sio kwa sababu hawapo, matajiri wanawake wapo, ila they are not registered kwenye jarida la forbers!.

Ikitokea ni kijijini, wanawake wote wanamiliki nyumba za nyasi, mwanamke tajiri kuliko wote ni yule mwenye kumiliki nyumba ya bati!. Na ikitokea wanawake wote wanatembea kwa miguu, mwanamke tajiri, ni yule mwenye kumiliki baiskeli!.Hivyo kwa muktadha huo, jee top ten wanawake matajiri waTanzania ni kina nani?!.
  1. Mercy Mengi-50% owner wa IPP Group of companies.
  2. Sabira Dewji-Binti wa Bilionea Gulam Dewji, mdogo wake Mo-Dewji.
  3. Dr. Getrude Rwakatare-Huyu ni mmiliki wa shule za St. Marys International Schools. Anamiliki prime lands karibu kila mkoa Tanzania. Source ya utajiri wake ni akili ya kutafuta ufadhili, akianzia na ujenzi wa kituo cha yatima Tabata.
  4. Rahma Al Kharoos, rais wa RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED.
  5. endelea.....
Tuwapongeze wanawake hawa kwa utajiri wao ambao pia unachangia kwa ustawi na maendeleo ya taifa!.
Pasco.
Update 2024
No. 1 na No. 3 wametangulia mbele ya haki.
No. 2 hasikiki tena, utajiri umeshikiliwa na kaka Mtu, Mo Dewji.
No. 5, hasikiki kabisa!.
Sasa Position No. 1 inashikiliwa na Angelina Ngalula a self made bilionea mwenye Agrocom na Bravo Logistics.
P
 
Huyo namba moja wako hebu chambua "akili ya kutafuta ufadhili" halafu uweke kwenye utajiri wake binafsi
 
Leo umenifikirisha sana Pasco. Wanawake matajiri watakuwepo, ila mfumo dume hauwatambui kirahisi. Mali zote ziko kwenye jina la mume. Kweli safari ipo.

Hivi yule mrembo jina linaniponyoka, mwenye lake oil sijui? Aliwapeleka twiga star USA kufanya tour na kuwafadhili hadi viongozi wakaanza kurushiana majungu. Nikumbushe jina lake
 
Last edited by a moderator:
Malkia wa Nyuki. Yule wa kampuni ya mafuta.
 
tutapigishana stori za vijiweni tu hapa. Ukweli ni kuwa data za utajiri ni ngumu sana kupatikana Africa.
 
Wanabodi, Leo ni Siku ya Wanawake Duniani, katika safari ya kuelekea usawa wa kijinsia, kuna wanawake wengi wenye akili, uwezo, na utajiri. Je wanawake kumi ambao ni matajiri wakubwa Tanzania ni kina nani, utajiri wao nini, na umetokana na nini?.Sehemu ya kwanza kupiga hodi ni kwenye jarida la forbers!.Huku sikukuta hata jina moja la mwanamke yoyote tajiri kutoka Tanzania!, hii maana yake, hatuna mwanamke yoyote tajiri mwenye viwango vya utajiri wa kimataifa, sio kwa sababu hawapo, matajiri wanawake wapo, ila they are not registered kwenye jarida la forbers!.Ikitokea ni kijijini, wanawake wote wanamiliki nyumba za nyasi, mwanamke tajiri kuliko wote ni yule mwenye kumiliki nyumba ya bati!. Na ikitokea wanawake wote wanatembea kwa miguu, mwanamke tajiri, ni yule mwenye kumiliki baiskeli!.Hivyo kwa muktadha huo, jee top ten wanawake matajiri waTanzania ni kina nani?!.
  1. Mercy Mengi-50% owner wa IPP Group of companies.
  2. Sabira Dewji-Binti wa Bilionea Gulam Dewji, mdogo wake Mo-Dewji.
  3. Dr. Getrude Rwakatare-Huyu ni mmiliki wa shule za St. Marys International Schools. Anamiliki prime lands karibu kila mkoa Tanzania. Source ya utajiri wake ni akili ya kutafuta ufadhili, akianzia na ujenzi wa kituo cha yatima Tabata.
  4. Rahma Al Kharoos, rais wa RBP OIL & INDUSTRIAL TECHNOLOGY (T) LIMITED.
  5. endelea.....
Tuwapongeze wanawake hawa kwa utajiri wao ambao pia unachangia kwa ustawi na maendeleo ya taifa!.Pasco.

Anna Tibaijuka, bilionea na mmiliki wa shule za Babro Johnsson, shule za wasichana zenye ubora wa kimataifa, utajiri wake sijui kwa kweli kaupataje.

Lady Jay Dee, mwanamziki na mmiliki wa mgahawa maarufu wa MOG na bendi ya muziki, utajiri wake unatokana na shughuli zake za muziki, anatembelea gari aina ya range rover spot lenye thamani kubwa.

Wema Sepetu, mwigizaji maarufu na mtu anaengoza kuandikwa na magazeti ya shigongo, anajipatia utajiri kutokana na mauzo ya filamu na shughuli binafsi.

Lulu, nayeye yumo, ila sijui utajiri wake kaupataje.
 
haa haa hadi lulu ni tajiri...anamiliki nini hapa mjini?
 
Back
Top Bottom