Siku yako ya kwanza kupima UKIMWI, ulikuwa katika hali gani?

Siku yako ya kwanza kupima UKIMWI, ulikuwa katika hali gani?

Requal

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2020
Posts
1,025
Reaction score
1,917
Nimeikumbuka leo nimebaki nacheka tu.

Ni siku ambayo haikuwa rahisi kabisa kwangu ilikuwa ngumu mno, ILINICHUKUA ZAIDI YA MIAKA MIWILI NIKIWA NA WAZO TU LA KWENDA KUPIMA NA SIKUWAHI KWENDA, lakini mambo yakawa mabaya zaidi nilipopata GF mpya aliyetaka tupime kwanza kabla ya kula tunda, nilitumia zaidi ya siku mbili naenda mwenyewe hospitali halafu nakimbia😀 na papuchi inasubiri tupime ndio ichakatwe.

Hapa nilitaka nihakikishe kwanza mwenyewe afya yangu, kabla sijamuita sijamuita huyu GF mpya tukapime wote

Mawazo ya Ma - ex wangu wanaojaza zaidi ya YOUTONG 8 na wengi nilikuwa sivai kinga yakaanza kujaa kichwani mwangu (mimi sio muumini wa condom mpaka sasa), bado wale wa kununua , nikawa naenda hosipitali nakaa kwenye foleni nakuwa busy kuongea na simu za uongo ikifika zamu yangu naona isiwe tabu najidai natoka nje kuongea na simu hapo ndio mazima.

Kipindi hiki mtoto mzuri anangoja simu yangu tu tukapime anipe papuchi, mimi nikawa namplease kwamba niko busy, kumbe nahangaika mahospitalini😀.. Siku moja nikajitoa mhanga nikapima japo nilikuwa natetema mpaka dktr aliyenipima akajua, sikuwa na utulivu wa akili kabisa.. Majibu yalipotoka sikuamini japo yalinipunguzia presha, nikaenda hospitali nyingine nikapima yakatoka kama ya mwanzo nikafurahi sana huku najisemea MOYONI, UKIMWI haupo hahaha ....nikachukua simu yangu kwa furaha kabisa nikamuita Nancy aliyekuwa ananingoja siku kadhaa tukapime ili anipe utamu.. tukaenda tukipma wote halafu tukagegedana kavukavu. Hii siku nilikuwa na furaha sana yaani nilikuwa mtu wa tofauti kabisa.

Ahsante sana Ex wangu Nancy ulibadili mfumo wangu mzima wa maisha ya kuchakata papuchi bila kupima😀

Tangu siku hiyo kabla sijagegeda lazima tupime hata iwe usiku nilikuwa natafuta hospitali za private natoa pesa tunapima, baadae nikawa na namba za madaktari kabisa ikitokea nawavutia waya tu napata huduma.

Kwa sasa serikali imeturahihishia tunatembea na HIV test tu.

wewe kwako ilikuaje?

N:B
UKIMWI UPO NA UNAUA, JIKINGE
 
Hivi kupima UKIMWI ni big deal eti?
 
Daah nimepima nimekaa kidogo kwenye kichumba kidogo doctor alipoweka kipimo changu namskia kama anaguna hivi


Daah hapo miguu kidogo ikaisha nguvu Mara paap doctor anakuja

Mr mlevi mmoja unaishi na nani ? .kipi kimekusukuma ucheki afya yako ?..maswali kibao nilitamani nimpige kelbu moja tu anipe majibu yangu maana maelezo yake yalikuwa mzigo kwangu [emoji3]


Daah kupima kweli kwataka moyo nyie kusikieni tuuh
 
Siku ya kwanza kupima walikuja watu wa damu salama shuleni kwetu, nilikuwa kidato cha tatu. Walirudi baada ya mwezi kutuletea majibu tuliojitolea damu. Nilikuwa na hofu kidogo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulienda kupima watu wanne afu kati ya watatu waliobakia kulikuwa na crush wangu mmoja hivi afu nilikuwa najiamini sanaa nikadhani majibu yakiwa mazuri labda nitaambulia chchte, majibu yalikuwa fresh na tulipewa kwa pamoja as a team ila bado haikuweza kudaka akili ya yule crush
 
Kuna bi mkubwa mmoja pale Angaza, mnazi mmoja Dar, alikunywa maji ya kilimanjaro 1.5L ndani ya dakika 20. Na hapo ni asubuhi saa mbili. Kila akitaka kwenda nje kupunga upepo, mmewe anamshika mkono asiondoke.

Na hapo ilikuwa wakati wa ushauri tu, bado kupima.
 
Ilikuwa Aghakan hosp nilienda na mchuchu miaka ile, mchuchu alikuwa msomi sana. Akaleta habari za kupima looh nikajiongeza ngoja niende mwenyewe nikajihukumu. Walitupima fresh wakati wa kusubiri majibu wakawasha Tv wakaweka kanda, looh hapo waliweka picha za ukimwi zile za Bukoba. Watu wameisha hatari nikamwita mmoja ya washauri nikamwambia uoni km unatutisha wkt hapa tunasubiri majibu.Nashukuru yalitoka fresh. Next wiki nikampigia mchuchu twende na macomfidence kibaoo. Tulipopima na ndoa juuu juu nikauwaga ukapela fasta
 
Kupima ukimwi sio big deal mbona, ts easy tyuh
 
Kwanza ardhi niliona inatetemeka kichwa kikawa cha moto nikaegemea dirishani nikajikuta nimevunja dirisha la kioo nikatumbukia ndani kule nikakutana na dokta anajianda na shughuli zake nikakumbana nae tukazoana haoo chini nikazimia, nafikili mtoa mada tuko sawa sawa🤦🤪😂🏃
 
Daah nimepima nimekaa kidogo kwenye kichumba kidogo doctor alipoweka kipimo changu namskia kama anaguna hivi


Daah hapo miguu kidogo ikaisha nguvu Mara paap doctor anakuja

Mr mlevi mmoja unaishi na nani ? .kipi kimekusukuma ucheki afya yako ?..maswali kibao nilitamani nimpige kelbu moja tu anipe majibu yangu maana maelezo yake yalikuwa mzigo kwangu [emoji3]


Daah kupima kweli kwataka moyo nyie kusikieni tuuh
Halafu siku hizi mbona hawatoi hata ushauri nasaha? Mimi mara ya mwisho kupima nilienda tu hospitali na ishu zangu tena sikuwa hata naumwa nilitaka tu kutega kazini. Kufika nikamwambia Dr naumwa kichwa... akaniuliza mara ya mwisho kupima VVU lini nikamwambia miaka 10 iliyopita, kaniandikia nikaenda kupima...hata wakati wa kutoa majibu wala hakuwa na maelezo yoyote.
 
Sijawahi na sitakuja kupima kamwe,,nikikumbuka sarakasi zangu yaani ndo nagwaya kabisa kupima,,,,mana wahenga wanasema unachokitafuta utakipata😀😀😀😀😀😀
 
Sijawai pima kwa hiari, mara zote imekuwa nikwasababu ndiyo masharti ya kupata ninachokitaka.
 
Dooh.. kumbe ata Nancy mwenyewe umeshambwaga..
 
Back
Top Bottom