Siku yangu ya kwanza kwenda USA yaliyonisibu

Siku yangu ya kwanza kwenda USA yaliyonisibu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Nilikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu, nilipata mualiko kutoka kwa mwanafamilia. Niliingia American Embassy nikajaza fomu wakati huo kila kitu kilikua manually. Baada ya kujaza fomu na kuikabidhi na passport yangu niliitwa dirishani na mama wa Kihindi. Aliniuliza maswali mengi ya course ninayosomea. Mwisho aliniambia tunafanya maamuzi mchana huu, acha pesa za kulipia gharama za kukurudishia passport yako ni courier service. Baada ya kulipia niliambiwa nirudi saa nane mchana. Nilizunguka mjini nikarudi sana nane. Niliambiwa tumekupa visa ya miaka miwili, katika hii miaka miwili una uwezo wa kuingia na kutoka bila kuja kutuona tena.

Niliondoka na British Airways enzi hizo mkitoka Dar mnatua Heathrow mnapata bus la kwenda Gatwick huko mnachukua pipa moja kwa moja USA. Kumbe katika masham sham ya safari nilisahau address ya mwenyeji wangu.

Immigration officer aliniuliza unakwenda wapi, sina jibu. Nilimwambia mwenyeji wangu yuko nje ananisubiri. Alisema ni lazima tufahamu unakwenda wapi.
Nilifanyiwa search si ya kitoto. Baada ya kuridhia kuwa sina madawa ya kulevya waliniita ofisini nikaulizwa ninataka kunywa nini. Nilipewa kikombe cha kahawa. Walinuliza jina la mwenyeji wangu na tarehe yake ya kuzaliwa waka run data base yao wakamuona. Walichukua details wakaniruhusu kuingia.

Nimetoka nje abiria wote wa ndege niliyoingia nayo wamshatoka, wenyeji wangu walijua niko detention. Waliponiona walifurahi sana.
 
Back
Top Bottom