Siku za kisukari, umaskini, wazee nk. zinatusaidia nini hasa?

Siku za kisukari, umaskini, wazee nk. zinatusaidia nini hasa?

Tikerra

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2008
Posts
1,702
Reaction score
147
Unajua, vitu vingine vinachekesha sana.Vinachekesha kwa sababu hii inaonyesha kwamba kabisa hatuna 'diagnostic minds.' Katika hali isiyo ya kawaida kabisa,hawa watu ambao ndio wanaopanga njama za kutuangamiza,wanatung'ong'a kwa kutuletea ujinga huu usiozungumzika.Eti siku ya umaskini duniani,kisukari nk.World Bank,IMF,UN na 'affiliates' zao' ndio wanaohusika na kupanga mikakati yote ya kuangamiza nchi zetu. Leo tuna shangilia kufanywa kuwa maskini, inatisha sana.'Evidence' ya haya ninayo ongea yako kila mahali,isipokuwa hatutaki kuona,kusikia wala kujua.Tutatapotaka kuona na kujua 'it will to late,'hapatakuwa na 'escape root.'We should stop this non-sense.'Tuache kushangilia matatizo yetu, na badala yake kama tuko 'serious', tutengeneze mikakati mizuri na ya kweli ya kuyatatua.Mawazo kwamba tusipoadhimisha siku hizo tutasahau matatizo hayo, hayana msingi wowote,'it's mere brainwashing.'
 
sawa, ni brainwashing. baadaye yatafuata maagizo ya wakubwa. zitaundwa na ngo za kushughulikia sherehe hizo za kila mwaka. sijui ni wazee wangapi wamesaidiwa na sherehe za wazee, au ni wagonjwa wangapi wamefaidika na sherehe hiyo ya siku moja.
waafrika ndivyo tulivyo. tunafuata wakubwa wanasema tufanye nini, hata kusherehekea.

macinkus
 
Sidhani kama siku ya kisukari, siku ya cancer duniani ni sherehe. Kwa kkawaida inatakiwa wataalamu wawaeleze watu ni nini dalili za magonjwa haya na ni jinsi gani unaweza ukapata tiba au ukajikinga na hayo maradhi. Wataalamu wanaweza wakaja makazini, kwenye zahanati mbali mbali na hata wanaweza wakaweka kambi sokoni na sehemu nyingine ambapo watu wengi hukutanyika including misikitini na makanisani. Tatizo linakuja tu kama siyo rahisi kuwakutanisha watu, hasa katika vijiji ambavyo population is sparse.
 
Back
Top Bottom