Hapa naamua kuwa OBJECTIVE, somo la history ndilo linalompa mtu "sprit of Patriotism "
Hiyo ni moja ya OBJECTIVE ya somo la HISTORIA.
Mathalani Kitendo cha MKWAWA,BWANA HERI,ABUSHIRI ,YUSUPH BIN OMARY MAKUNGANYA,KINJEKETILE, Kuupinga utawala wakoloni kwa kuchukua silaha.
Wanafunzi wansposoma ,wanahamasika kabisa ,wanakuwa inspired kuipigania nchi, kuipenda wakitumia mfano mzuri wa hao mashujaa waafrikawaloishi miaka ya 1880's
Mh Rais kama kazungumzia kuwa somo la history linawajenga watu kuwa wazalendo YUPO SAHIHI asilimia 100%.
Kuhusu Civics somo la Uraia kiasi kikubwa linabase kwenye haki za Raia na wajibu.
MIMI NI MWALIMU MTAALAMU WA MASOMO HAYO MAWILI.
2018 nilifaulisha civics na darasa langu lilikiwa 20 kitaifa,2019 History tena 20 kitaifa.
Nimetoa maoni kama Mtaalamu mbobezi katika masomo hayo.
Katika kauli ya Rais yupo sahihi 100% tusiwe tunampinga kwa kila kitu,mambo mengine tuwe OBJECTIVE.
UKANA SHILUNGO.🙏🙏🙏
Yes, your President is right 100%...
Nionavyo mimi ni hiki, kuwa, mleta mada na wewe kuna point mnai - miss...
Kwamba, ishu siyo kukubaliana au kutokukubaliana kufundishwa somo la Historia ya Tanzania kwa sababu inafundishwa hadi sasa...
Chukua mtaala na muhitasari wa somo la Uraia (Civics) Shule za Sekondari. Kidato cha kwanza kuna mada ya "OUR NATION" ikieleza historia ya Taifa letu (Tanzania) kwa undani na ufasaha sana...
Mwanafunzi huyu huyu akiingia kidato cha II atakutana na mada inayokazia mambo haya haya (historia ya Tanzania) ktk mada ya "OUR GOVERNMENT" ambamo ndani yake atafundishwa mpaka UNION OF TANGANYIKA & ZANZIBAR na sababu za muungano huo..
Haishii hapo tu, bali atafundishwa mpaka KATIBA YA TANZANIA sura kwa sura na ibara kwa ibara pamoja na HUMAN RIGHTS na DEMOCRACY kwa ujumla. Swali la kujiuliza la watu kutokuwa wazalendo ni kwa sbb wanafunzi hawafundishwi somo la Uraia kwa Kiswahili au ni nini...?
Mimi nadhani maswali ambayo ningependa tuyajibu wote katika mjadala huu ni haya mawili au matatu;
1. Kama ishu ni HISTORIA YA TANZANIA tayari inafundishwa kwa ukamilifu wake ktk masomo ya Historia yenyewe, Uraia/Siasa na Maarifa ya Jamii. Sasa kwanini, hiki kinachodhaniwa ni tatizo la Uzalendo miongoni mwa Watanzania, lipo pamoja na kufundishwa historia yao...?
2. Je, tunadhani tatizo ni historia hii kufundishwa kwa Kiingereza badala ya Kiswahili kiasi cha kuanzisha somo la Historia ya Tanzania kwa Kiswahili na kudhani hilo ndilo litakuwa suluhisho..?
3. Kwa maoni yangu, tatizo la nchi yetu si watu kutokuwa wazalendo kwa nchi yao. Ni tatizo la tafsiri ya "UZALENDO" kutofautiana kwa wanavyoelewa viongozi na vile wanavyoelewa wananchi wanaowaongozwa na viongozi hawa...
Hapa ndipo ilipo shida na mikwaruzano yote hii ya tofauti ya kimitizamo kati ya tabaka la watawala (viongozi) na watawaliwa (wananchi)...
Viongozi wetu hawa wa kuchaguliwa tafsiri ya "uzalendo" kwao ni wananchi kuwapenda viongozi wao bila kujali chochote. Kutofanya hivyo, kwao wananchi hao wanakuwa hawana uzalendo na lazima itafutwe namna kuwafanya wawe wazalendo...
WAKATI;
Sisi wananchi tunaamini kuwa, maana na tafsiri ya "UZALENDO" ni mtu kuipenda nchi yake na kuwa tayari hata kuifia. Na hii kiuhalisia ndilo lipo ndani ya mioyo ya wananchi karibu wote wa nchi hii...
Wanachofanya viongozi wetu hawa kwa sasa akiwemo Rais Magufuli mwenyewe ni kujaribu kuitoa mbegu hii ndani ya mioyo ya watu na kupanda mbegu nyingine ya wananchi kutukuza na kupenda viongozi wao badala ya nchi na kwamba hiyo ndiyo iwe maana na tafsiri mpya ya "UZALENDO"...
Huu ndiyo msukumo uliopo nyuma ya hiki kinachoendelea na kinachotaka kufanyika sasa kuanzishwa kwa kinachoitwa somo jipya la HISTORIA YA TANZANIA eti kufundisha watu UZALENDO...
Lakini ukweli ni kuwa kuna watu wanataka kuandikwa na majina yao yatumike kutajwa huko mashuleni. Nothing more, Nothing less...