Sikubaliani kabisa na utaratibu wa Serikali kuwataka wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ilihali imetumia bilioni 700 kujenga daraja

Sikubaliani kabisa na utaratibu wa Serikali kuwataka wananchi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa ilihali imetumia bilioni 700 kujenga daraja

Hata zile pesa zilizotumika kununua Madiwani na Wabunge Nchi nzima, zingetosha kuongeza Madarasa Nchi nzima!
Walikuwa wananunuliwa kwa mamilion ya pesa, zote walizoinvest kwenye uchaguzi huku wakijua kuwa wataiba kura haikuwa na maana. Sasa wanaanzisha kodi mbalimbali na kuwalazimisha wananchi wachangie garama za kujenga madarasa watakaoshindwa kuwasweka rumande. Tuliyataka wenyewe
Mitano teeeena au nasema uongo jamani?
 
Ilitakiwa wananchi tuchangie ujenzi wa madaraja halafu serikali ijenge madarasa kwa fedha za mapato ya ndani

Kwani serikali si inajinasibu kilasiku kuwa ina pesa za kutosha? Kwanini tuongezewe kodi na kulazimishwa kuchangia ujenzi wa madarasa? Yaani it's key responsibility to the public is to ensure people are getting better social services period.
 
Sasa unataka nani ajenge mkuu,
Serikali, kwani majukumu yake kwa wananchi wake hayajulikani?
Msiwafanye wananchi maboya wakati mnatukamua kodi kupitia vyanzo mbalimbali. Tena msijitoe akili kabisa hao wanaojitolea kuchanga mkawaona machizi au majinga flani, mnadhoofisha elimu ili kukuza ujinga na kukutumia kuendelea kutawala. Mungu awalaani
 
Vipi wale waliowataka wananchi masikini wachangie mikutano yao ya kisiasa huku wakiwa tayar wameshakusanya mamilioni ya michango wa wabunge jumlisha na ruzuku ya chama iliyokuwa inakusanywa kila mwezi? Au lile la michango ya mikutano ya siasa haukuliona?
Tulichangia kwa hiari yetu hakuna aliyetulazimisha
Ulitaka tuwachangie wanaonunua wabunge
Fedha ni zetu na uamuzi ni wetu

Mnataka mtupige na mtufundishe kulia?
 
Serikali ilisema itatoa elimu bure, kwamba mwananchi asitozwe mchango wowote.....sasa sijui tumefika vipi hapa.
 
Nimejuliza hivi hilo daraja linahudumia Watu wangapi? hivi isingewezekana kuweka kivuko cha kisasa tu kisichozidi hata milioni mia mbili au tatu?.

Ifike mahali miradi ijadiliwe kwanza na ipimwe tija yake kabla ya kutekelezwa.
 
Back
Top Bottom