Sikubaliani na Harakati za GSM za Kumleta Cloatus Chama Jangwani (Yanga SC)

Sikubaliani na Harakati za GSM za Kumleta Cloatus Chama Jangwani (Yanga SC)

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Najua GSM imekuwa kwenye pilika za kumleta Chama Jangwani tangu kitambo. Tangu alipokuwa ukingoni mwa mkataba wake na Simba, kabla hajaongezewa mkataba mpya.

Na sasa kuna jitihada za kumrudisha Bongo ajiunge na Wanajangwani. Eng Hersi Said amehusika pakubwa katika kumshawishi Prof Coach NABI aonyeshe nia ili uongozi ufanye mchakato wa kumleta.

Nasikia mmeanza jitihata za kuhakikisha dirisha asajiliwe haraka iwezekanavyo.

Kwa mtazamo wangu binafsi sioni umuhimu wake kwasababu katika nafasi yake tunaye Feisal Salum. Cha ajabu pia tuna Aucho ambaye anatimiza majukumu sawa ya kuanzisha mashambulizi.

Chama wa nini?

Hizo pesa kwanino msiziwekeze kwwnye maeneo mengine klabuni?

Tatizo la kiufundi tulilo nalo hivi sasa ni kukosekana kwa washambuliaji wa pembeni wenye uwezo wa kwenda uso kwa uso na mabeki.

Kwanini tusiwekeze hizo pesa kwenyw eneo hilo basi..?

Tisifanye sajili kwa lengo la kukidhisha kiu ya kihisia za mashabiki..bali tuangalie kwa uwanda mpana zaidi.

Kwa heri wana Jamvi.
 
Furaha ya Yanga ni tetesi kama hivi hasa zenye kuhusu Simba na kwa sasa nahisi GSM kashatembeza mpunga kwa Wachambuzi chawa waanze kuhype hii tetesi. Hii tetesi itapamba moto mara tu pale Yanga akipoteza game
 
Akuna uhakika wa 100% wa icho unachokisema, msije mkaingia kwenye mtego wa wahandishi wa habari wanaopenda kuuza magazeti yao na blogers kwa habari za uhongo, yanga kumpata chama inategemea simba waliomuuza kama awakuweka kipengele cha kutomuuza kwa timu yoyote apa Tanzania isipokuwa wenyewe simba Kama berkane wakitaka kumuuza, au nje ya nchi nyingine, maana hivi vilabu kwa sasa vimekuwa makini kwenye mikataba ili visihujumiane kwenye masuala ya usajili, sasa Kama icho kipengele akikuwepo basi Yanga wanayo nafasi ya kumpata na kama icho kipengele kilikuwepo yanga awawezi kumpata kamwe labda kuendelea kupiga porojo tu siku ziende.
 
Yanga kumpata chama inategemea simba waliomuuza Kama awakuweka kipengele cha kutomuuza kwa timu yoyote apa Tanzania isipokuwa wenyewe simba Kama berkane wakitaka kumuuza.
Kama hawajaweka kipengele hiko?

Na kwanini kipengele hiko kimewekwa kwa Miqquisone kama Simba wana amini kuwa Yanga SC hawana uwezo wa Kumchomoa kutoka Al Ahly?
 
Najua GSM imekuwa kwenye pilika za kumleta Chama Jangwani tangu kitambo. Tangu alipokuwa ukingoni mwa mkataba wake na Simba, kabla hajaongezewa mkataba mpya...
Acha tu aje kama itawezekana ili dhana ya kikosi kipana itimie! Kuna dalili akikosekana Dr. Khalidi pila biliani kutonoga!
 
Uwezo huo hawana.
Uwezo Gani?

Unajua kwanini kwenye dili la Miqquiesone kwenye mkataba Simba/AlAhly kuna kipengele ambacho hakimruhusu kununulia na klabu yeyote ile kwenye Ligi Kuu Tanzania ndani ya miaka 5...?


Kuwa na siku njema.
 
Kama hawajaweka kipengele hiko?

Na kwanini kipengele hiko kimewekwa kwa Miqquisone kama Simba wana amini kuwa Yanga SC hawana uwezo wa Kumchomoa kutoka Al Ahly?
Ndo nakwambia inawezekana kipengele walichokiweka kwa miquison ndo icho icho walikiweka kwa chama, sio kwamba yanga wanashindwa kumchomoa wanamchomoa ndo maana wakajilinda kwa staili iyo wasije wakamuuzia adui siraha
 
Kukujibu swali lako na wewe ukaridhika itanipàsa kwanza ku-reveal true identity yangu..



Sito fanya hivyo!
But mkuu usiangaishwe na tetesi,kingine watu wa Yanga tujitahidi tuwe wasiri na mambo yetu sio kila tunachokisikia tunakimbilia kwenye public
 
Back
Top Bottom