Sikubaliani na hiki alichofanyiwa huyu binti, Jeshi la Polisi lichukue hatua kwa waliohusika

Sikubaliani na hiki alichofanyiwa huyu binti, Jeshi la Polisi lichukue hatua kwa waliohusika

Hata biblia ilihalalisha viboko acha apapaswe ila wanachokosea ni ulimbukeni wa maclip yao afu yanawacost.......kanisa waumini ni wadhaifu mnoooo katika imani yao...hao wezi ndo wanaitaji msaada wapate kupona uyo mama anafukuza kabisa eti usirudi tena hapa yaan sjui wanamuomba Mungu gani na wanasoma biblia zipi wote wapumbavu kabisa
 
Huyu mama wa pembeni ninamashaka na matendo yake kwa hii kauli yake ya kusema eti ""bint mzuri afu unaiba""....aisee afu anaonekana ni mama mchungaji

Hv sadaka na zaka si kwaa ajili ya maskini na mafukara.... ahahaa wazee wanahasira na mitaji yao
 
Kasomeni maandiko viboko vimeruhusiwa katika kumuweka mtu sawa ....ova proudly Anglican😇
 
Kuna jamaa alikuwa mwizi wa magari yeye alikuwa anaiba magari ya kabisa na ya Serikali tu.anasema hizo Taasisi ndizo hazitafuti kwa jasho.
 
Kuna Jamaa yangu niliwahi kumpatia Laki na Sabini aninunulie mzigo flani, akaanza kunizungusha na kunikwepa mpaka nikaamua kusamehe pesa yangu.

Majuzi hapa nakutana naye ananiambia ameshakuwa Mchungaji na tayari ana mahali kaanzisha kanisa.

Sasa Mchungaji wa namna hii ukiingia anga zake hawezi kupata tabu kukulamba makofi.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Kuna Jamaa yangu niliwahi kumpatia Laki na Sabini aninunulie mzigo flani, akaanza kunizungusha na kunikwepa mpaka nikaamua kusamehe pesa yangu.

Majuzi hapa nakutana naye ananiambia ameshakuwa Mchungaji na tayari ana mahali kaanzisha kanisa.

Sasa Mchungaji wa namna hii ukiingia anga zake hawezi kupata tabu kukulamba makofi.
 
Huyo binti ilibidi atolewe pepo la wizi na kumbadilisha kwa maombi awe raia mwema sio kumpiga.

Makanisa ya sasa hayana nguvu za Mungu yapo kibiashara zaidi ndio maana yanachukia kuibiwa badala ya kubariki na kuombea wanaowaudhi kama huyo mwizi.
Mwenyewe nimeshangaa Sana na huku wao wamekomaa kuwa usihukumu.ukichukuliwa shati toa na koti ama ukipigwa huku geuza na kule
 
Huyo binti ilibidi atolewe pepo la wizi na kumbadilisha kwa maombi awe raia mwema sio kumpiga.

Makanisa ya sasa hayana nguvu za Mungu yapo kibiashara zaidi ndio maana yanachukia kuibiwa badala ya kubariki na kuombea wanaowaudhi kama huyo mwizi.
Umeongea point kubwa, kama wao ni waumini wa imani ya kweli basi wangemuombea pepo la wizi limtoke, kumpiga maana yake hawana uwezo wa kuwaombea wenye matatizo.
 
Kumekua na Video inayozunguka katika Magroup ya Whatsapp na mitandao mbali mbali.

Video ikimuonesha binti anayetuhumiwa kwa wizi katika makanisa.

Viongozi/waumini wanaonekana katika video hii wakimpiga mtuhumiwa.

Jambo hili halikubaliki na niuvunjaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Kama hawa ndo viongozi wa dini, basi tuna safari ndefu kama taifa.

Natumaini kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Video yenyewe hii hapa. View attachment 1807236
Hilo ni kosa kubwa kwa kuchukua sheria mukononi mwao lakini wamekosa roho ya kusamehe na hawana uhalali wa kuwaomba waumini wao kuwa masamehevu
 
Kumekua na Video inayozunguka katika Magroup ya Whatsapp na mitandao mbali mbali.

Video ikimuonesha binti anayetuhumiwa kwa wizi katika makanisa.

Viongozi/waumini wanaonekana katika video hii wakimpiga mtuhumiwa.

Jambo hili halikubaliki na niuvunjaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Kama hawa ndo viongozi wa dini, basi tuna safari ndefu kama taifa.

Natumaini kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Video yenyewe hii hapa. View attachment 1807236
Tena hapo Kuna dada anaongea kikatili sana na huku ni mdada.yaani jamani Hawa jamaa hata hawajui kuwa wanafuata Nini kwenye nyumba za ibada. Ni kwa Nini uhukumu na huko sijui ni RC wanakotangaza mapendo daima. Bora wangemchukua wakamtafutia kazi wakamsaidia.
Ndo mie Mimi Keisangora wa Tanzania. Huwezi nishawishi kuwa niende kanisani. Ibada ni matendo yako ya kila siku unavyomtendea unayekutana naye machoni pako. Pia Mungu ni upendo full stop.
Zingine zinakuwa ni Saccos na watu kufahamiana.jumuia za kuchangiana michango na wengine waishi vyema
 
Hii nchi wajinga wengi. Kweli dada katenda kosa kaiba halafu hayo malokole yalivyo na akili hovyo badala ya kumpeleka polisi yanachukua sheria mkononi huku yanajirekodi video na visimu vyao vya kichina. Huo ni ushamba wa hali ya juu sana. Hapo tayari wana makosa kibao ;- kuchukua sheria mkononi, udhalilishaji wanaofanya hao wanaume dhidi ya huyo binti, shambulio kwa kutumia fimbo na kumrekodi halafu kurusha mtandaoni. Huyo binti japo kakosea lakini akipata mwanasheria mzuri hao jamaa pamoja na huyo dada kiherere anayezungumza hapo hawachomoki hata mmoja. Yale yale ya maofisa uhamiaji yanajirudia hata wiki haijaisha. Hiyo kwa watoto wa mjini wanakwambia "ushahidi ubaoni kwa hakimu" kesi imeshaisha kabla hata hakimu haijaita mashaidi.

Haya watu wa haki za binadamu na watetezi wa wanawake kazi kwenu kumtafutia huyo binti haki yake. Kweli nimeamini adui wa mwanamke ni mwanmke mwenyewe.
 
Watasingiziwa walokole naona kama wakatoliki hapo. Sadaka sadaka
 
Ndipo yesu kasema samehe saba mara sabini....cha kushangaza wazee wa kanisa wameshindwa kumsamehe binti mwizi...ila nimependa huyo dada anavyosisitiza msimpige kichwani anaonyesha kumjali.
 
Kumekua na Video inayozunguka katika Magroup ya Whatsapp na mitandao mbali mbali.

Video ikimuonesha binti anayetuhumiwa kwa wizi katika makanisa.

Viongozi/waumini wanaonekana katika video hii wakimpiga mtuhumiwa.

Jambo hili halikubaliki na niuvunjaji mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Kama hawa ndo viongozi wa dini, basi tuna safari ndefu kama taifa.

Natumaini kuwa sheria itachukua mkondo wake.

Video yenyewe hii hapa. View attachment 1807236

Neno linasema:

Usihukumu utahukumiwa
 
Back
Top Bottom