Sikubaliani na watu wanaoamini Fid Q ni genius

Sikubaliani na watu wanaoamini Fid Q ni genius

Hussein Massanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
1,016
Reaction score
2,195
Humu leo sijui kama patatosha!

Nimekuwa nikijaribu kudigest sifa ambazo wadau wengi wamekuwa wakimpatia msanii Fid Q, kwamba ni mtu makini, mwenye upeo wa hali ya juu.

Kiukweli nimejitahidi sana kuamini lakini leo acha tu niseme ukweli..

Mwaka jana mwanzoni, huko Marekani alitokea mtoto wa miaka 14 aliyebuni saa ambayo ilikuja kudhaniwa ni bomu hivyo kumkamata na kumtia kizuizini kwa masaa kadhaa kabla ya kubainika kuwa ni saa tu isiyo na madhara na baadae kuitwa Ikulu na Rais Obama kupongezwa kuwa ni genius.

Nilichopenda kwenye mkasa huo, ni jibu la mwalimu wake pale alipoulizwa kuhusu 'ukipanga' wa huyo mtoto na anajisikiaje kufundisha mwanafunzi genius darasani kwake.

Alisema hivi, "Namjua vizuri Ahmed, sio mwanafunzi genius kama inavyodaiwa, ila ana jitihada sana ya kusoma na kujifunza.

Jitihada zake ni zaidi ya wanafunzi wote ninaowafundisha".

Sasa hii ni kama ambavyo Fid anatajwa kuwa genius kutokana na uandishi wa tungo zake.

Kwamba anafikiria sana na ni kichwa kuliko wasanii wote.

Niseme ukweli, binafsi sikuwahi kuona hivyo, bali nimekuwa nikimwona kama msanii anayejitahidi sana kujifunza kuliko wasanii wengine.

Hapa tusichanganye.

For someone to be genius, ni lazima awe innovative! Lazima aache impact.

Ni bora nikamfagilia Mwana FA angalau yeye ameacha misemo mingi kwenye lugha ya Kiswahili.

Kituko hiki hapa sasa..

Nikki wa Pili alipouliza swali kuhusu kwanini vichaa hawaongozi kuugua kipindupindu licha ya kula vyakula vichafu, Fid anajibu ni suala la Kisaikolojia.

Eti, akili yako ukiiambia kwamba nikila hiki chakula kichafu nitaugua, utaugua kweli.

Na ukisema sitougua, hutougua.

Hivyo vichaa hawana hiyo time ya kujua kama ni kichafu ndio maana hawaugui.

Nilichoka.

Huo ni mfano mmoja tu. Mwingine nitajazia kadri mada hii itakavyoendelea.

Poleni kwa kusoma mkeka!
 
Haya hebu tuangalie definition ya neno "Genius" kutoka kwa wazungu wenyewe

Cambridge

very great and rare natural ability or skill, especially in aparticular area such as science or art, or a person who has this:

Oxford
1. Exceptional intellectual or creative power or other natural ability:
2. An exceptionally intelligent person or one with exceptional skill in a particular area of activity:
3. The prevailing character or spirit of something:

Mimi namuingiza kwenye Ugenius kwa hiyo definition number mbili ya Oxford...Na haswa hapo kwenye "Exceptional Skill in a particular area of activity"...Na the guy ana Exceptional skill katika hip hop...

Turudi kwenye definition yako..
"For someone to be genius, ni lazima awe innovative! Lazima aache impact"

Hii umeitoa kwenye dictionary gani?...Huo mfano wako wa kujibu swali la kipindupindu sio relevant maana genius sio lazma ajue kila kitu katika aspect zote za maisha...Hata mvumbuzi wa umeme ungemuuliza kuhusu kilimo cha tumbaku asingejua..

Acha kuwa Hater mkuu...The guy IS a genius...(Based on Oxford Dictionary)
 
Unakariri statement ya mwalimu kumjudge mtu!!! Hujiu kitu kuhusu falsafa ya maisha ya being !!!
 
kwenye hiyo video, Nikki ndio kaonekana mburula afadhali ya Fid....
Fid sio genious ni kweli. Nikki II sio genious ni kweli.
 
Haya hebu tuangalie definition ya neno "Genius" kutoka kwa wazungu wenyewe

Cambridge

very great and rare natural ability or skill, especially in aparticular area such as science or art, or a person who has this:

Oxford
1. Exceptional intellectual or creative power or other natural ability:
2. An exceptionally intelligent person or one with exceptional skill in a particular area of activity:
3. The prevailing character or spirit of something:

Mimi namuingiza kwenye Ugenius kwa hiyo definition number mbili ya Oxford...Na haswa hapo kwenye "Exceptional Skill in a particular area of activity"...Na the guy and Exceptional skill katika hip hop...

Turudi kwenye definition yako..
"For someone to be genius, ni lazima awe innovative! Lazima aache impact"

Hii umeitoa kwenye dictionary gani?...Huo mfano wako wa kujibu swali la kipindupindu sio relevant maana genius sio lazma ajue kila kitu katika aspect zote za maisha...Hata mvumbuzi wa umeme ungemuuliza kuhusu kilimo cha tumbaku asingejua..

Acha kuwa Hater mkuu...The guy IS a genius...(Based on Oxford Dictionary)
Shikamoo mzee kweli na wewe n genius akikataa mtu akwende zake
 
Umenichanganya unapozungumzia mambo ya kipindupindu na muziki...yaani unataka mtu mwenye upeo mkubwa kwenye sanaa anatakiwa awe na upeo mkubwa pia kwenye uelewa wa masuala mengine kama afya??..na huyo mwalimu wako wa marekani ni nani hasa kwenye dunia hii ndio mpaka jibu lake kuhusu mwanafunzi wake liwe hitimisho la utambuzi wa vipaji vya watu??..
 
U"genius " wa mtu upo kwenye eneo maalaum, iwe darasi, kwenye michezo au chochote kile.. Sioni sababu ya kumuona fid ni kilaza kisa jibu hilo, wee ushajiuliza hilo swali!!? Umepata jibu gani!!
Prof wetu lipumba, kabukua mpka na alikuwa t.o angalia anachofanya sasa hv mtoto mdogo hafanyi.. Unadhan kwakuwa messi ni genius wa mpira ndio atakuwa genius kote kote..

Tena hilo swali kajibu fresh tu, hebu jaribu kupima jibu lake usahihi wake, chukua embe mbov kula ukijua mbovu, halaf utaona kama tumbo halijakuuma, utahisi chochpte kile.. Then kumbuka siku uliyokula kitu kizima then baada ya siku kadhaa ukaja kujulishwa ulichokula hakikuwa kizima, uone kama uliumwa..

By the way kama humkubali fid hatukushikii bunduki, we ni mtu mzima na hayo ni mawazo yako, tunayaheshimu pia.
 
Back
Top Bottom