Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Waungwana!
Leo nilikuwa kwenye interview kama mnavyojua kijana ni taifa la leo, na kijana ni nguvu kazi ya nchi. Nami nikasema nisibweteke mwishowe nisijeitwa majina mabaya. Acha nitafute kazi hata zile nilizoona hazihitaji Vyeti. Maana hizo za Vyeti kiukweli Ngoma ngumu, nimeomba mpaka sasa nimekuwa mwombaji sugu.
Umri unaenda, bado sijaanzisha familia kwani sina kazi. Nikasema kazi ni kazi bhana! Ndipo nikavutiwa na kazi ya Uchawa. Mwanzoni niliidharau Kwa kufuata mkumbo tuu lakini nilipokuja kuchunguza kwenye huo mkumbo wengi wao wanakazi na wanavipato.. mmh! Nikaona hapa ninapotezwa.
Nikaona niingie kwenye Fani ya Uchawa Kabla macho ya Watu hawajaiona Hii fursa.
Ndio nikaenda Kwa huyo Mkurugenzi ambaye ni Kiongozi wa kitaifa. Huko nikakuta kumbe sio Mimi pekeangu niliyewaza hivyo.
Nilikutana na msururu WA vijana ambao walinishangaza Sana. Walivalia vizuri ungedhani wanaenda kuomba kazi ya Uwakili, walikuwa wamebeba na mabahasha ya kaki yaliyotuna, sijui ndani ya yale mabahasha kulikuwa na manini., nilipowauliza wanafanya nini pale wakaniambia wamekuja interview ya Kazi ya Uchawa. Nikabaki mdomo wazi. Kumbe nilipolalia wenzangu waliamkia Jana yake.
"Mpaka Uchawa tunaandika barua?" Nilijikuta nasema Kwa Sauti ya Chini nikiwa nimepewa barua na msahiliwa mwenzangu, nikiwa nasoma Sanduku la posta la mwombaji, sijui ilikuwa SLP ngapi, lakini ninachokumbuka ni title ya barua, Yah; maombi ya Kazi ya Uchawa katika Taasisi yako tukufu" Dooh!
Sikujua kama mpaka Uchawa unamambo haya. Kweli mambo yapo Taiti.
Hapo kwenye CV ndio nilibaki mdomo wazi. Jamani! Jamani! Hata Mkurugenzi WA umoja WA mataifa Hana CV kama Ile.
Mimi sijawahi kuona CV iliyosheheni kama Ile. "Haiwezekani kabisa"
Dakika kumi na tano kuipitia Ile CV juujuu kwani kama ningeisoma yote ingenimalizia muda. Nilivutiwa na kipengele cha Work experience pamoja na Language Skills, kwenye Lugha Yule mshikaji anajua Lugha tatu mbali na Kiswahili, anajua kingereza, kiarabu na kifaransa na zote ni Fluently.
Mimi mwenyewe licha ya kuwa Msomi tena sio usomi wa kuokoteza okoteza Bali usomi uliotukuka lakini kingereza kinanipiga chenga. Sasa iweje huyu chawa ajue Lugha zote hizi.
Nikasema Acha nimpime kama kweli yaliyomo yamo? Daah! Nilijuta. Sikuwahi kufikiri kuwa wapo machawa hatari kuliko hatari yenyewe.
" Sasa Taikon angalia usijekosa mpaka huku sasa" nikawaza huku nikimeza rumba la mate kisha nikamrudishia CV yake nikiwa ninahasira nisijue zilipotokea, sijui zilikuwa ni hasira za kukata tamaa au hasira za Wivu. Mimi sijui.
Ila Ndugu zangu, kama imefikia huku basi sijui itakuwaje,
Niliwahi kwenye Udalali nikakuta pako Full, nikaja kwenye Uchungaji wa upako Huko ndio nikaona nilichelewa, nikarukia kwenye betting huko nilikuta maajabu, kila sehemu ni nyomi.
Sasa nilipoona chimbo la Uchawa nikajua bado fani ni mbichi kumbe nimechelewa.
Ila nimeshapata wazo jingine, silisemi nisijeshtua Nzi, hapa nikikosa walahi wabinlah nanunua sumu ya panya.
Taikon nimemaliza.
Nawatakia Sabato NJEMA.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam