Paspii0
JF-Expert Member
- Apr 10, 2020
- 638
- 1,043
Kwa unyenyekevu na matumaini wanazuoni wenzangu, heshima sana kwenu...............
Sherehe za Pasaka zinatufundisha kila mwaka kuhusu maadili ya kujitolea, ukweli, na dhamira. Pasaka ilitokea baada ya Yuda kumsaliti Yesu kwa fedha za dhihaka, lakini pasaka sio tu kumbukumbu ya tukio la kihistoria. Ni kielelezo cha mabadiliko ya kiroho, wito wa kujitolea na kujenga dhamira. Tunapoangalia Pasaka, tusikubali kuwa sehemu ya yule Yuda Iskariote ambaye aligeuza ahadi za imani kuwa vipande 30 vya fedha. Katika maisha yetu, tunakutana na viongozi wanaokuja kwa ahadi, lakini baada ya kupata kile wanachotaka, wanawatupa kando, ni roho ya usaliti, na dhambi ya kutojua wajibu wao.
Wananchi, tutafakari kwa undani ni dhambi kutotimiza wajibu wetu. Kila mmoja wetu amepewa haki ya kupiga kura, lakini hii si haki peke yake; ni wajibu mtakatifu wa kutunga na kusimamia mustakabali wa taifa letu. Kutoruhusu haki hii ni kama kujifunga macho mbele ya fursa ya mabadiliko. Tunaposhindwa kutimiza wajibu wetu kwa taifa, tunatengeneza kivuli cha usaliti kwa vizazi vijavyo. Hivyo wananchi uchaguzi ukifika usipoteze haki yako na usitende dhambi ya kutopiga kura ni dhambi ya kutotimiza wajibu.
Wapiga kura ni wema wa taifa, lakini wale wanaokataa kushiriki katika uchaguzi wanazikalia sauti zao, wakikosa kugusa nafasi yao katika historia. Kila kura ni kielelezo cha dhamira, na ni sehemu ya mchakato wa kujenga taifa letu lenye msingi imara. Kuwa na dhamira ya kupiga kura ni kumtumikia Mungu na taifa letu, kutekeleza wajibu wetu kwa ajili ya vizazi vijavyo, na kutoa sauti ya haki na ukweli.
Pasaka inatufundisha kuwa uaminifu na kujitolea ni vipengele vya dhati katika utendaji wa binadamu. Tusikubali kuwa sehemu ya Yuda wa kisasa anayekuja kwa ahadi na kuondoka na mbinu za kisiasa. Watu hawa hufanya ahadi kwa ustadi wa kusema, lakini wanashindwa kutekeleza. Tuchague kwa hekima, si kwa mapambo ya ahadi, bali kwa njia ya ukweli.
Pasaka na uchaguzi ni fursa mbili za kutimiza wajibu wetu kama watu wa Mungu na kama wana wa taifa hili. Tusikubali kuwa sehemu ya mchezo wa usaliti, bali tuwe sehemu ya mabadiliko. Tuchukue hatua kwa dhamira na haki, tukiishi na kutenda kwa mfano wa imani iliyo hai. Huu ni wakati wa kutimiza wajibu wetu, kwa ajili ya taifa letu, kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki taifa letu.