OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Tukiweka ushabiki pembeni kuna mambo ya kuionea huruma sana Yanga. Moja kati ya hayo ni usajili wa Tuisila Kisinda.
Nakukumbusha tu kwamba huyu ndiyo mchezaji aliyewalipisha faini Yanga huko CAF ili atumike kimataifa. Huyu ndiyo yule aliyeifanya TFF iingie kwenye aibu kuhusu usajili wake. Huyu ndiye TK Master?
Inatia simanzi sana kuona pamoja na yote hayo badala yake amekuwa mtu wa mbio tu kama Linesman.
Katika mechi alizocheza sijaona cha maana zaidi ya mbio tu mpaka anapitiliza.
Wabongo tupunguze shobo na wachezaji wa nje. Kinyume na hapo tunaenda kuwa dampo la wachezaji