Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

kwa iyo wale ambao tumepima tukakutwa tumeathirika Mungu hatupendi na sio mwema kwetu..si ndio!!
in this life jaribu kujifunza kwamba kila kitu kinatokeakwa sababu ambazo wewe au mimi hatuzifahamu.......hakuna mtu asiependa uhai wake;wewe ulienusurika kuambukizwa haimaanishi ndio mwisho wa kutoambukizwa.........utaishi utasahu na litatokea lingine tofauti na hilo n aukajikuta upo positive......mshukuru Mungu kwa kila jambo.
watu wenye upeo na uelewa wa mambo kama wewe hatutegemei kuanza stigma na kujiona ndio bora kuliko hao walio positive....
ujumbe wangu:
hata walioathirika walikua Negative kama wewe!

hongera kwa kua negative...hata ukikutwa positive miaka 6 ijayo....umshukuru Mungu pia.. na maisha yaendelee!!
 
Smilenashukuru kujitolea kuniombea,kwakweli nitafurahi nikipata huo ujasiri
 
Last edited by a moderator:
@fazaa unapenda kucritisize kila kitu
Si kweli, hebu toa point au pin point wapi nime critisize everything

...huwa unajiona upo salama saaana na umebarikiwa kuliko watu wote kwenye mapenzi..gud for u
Wapi niliposema nimebarikiwa kuliko watu wote, mbona unasema vitu ambavyo sijavisema.

...but kumbuka mapenzi ni watu wawili na kila mtu ana moyo wake pia ni ngumu kuujua moyo wa mtu
Najua mapenzi ni watu wawili ndo mana kukawa na mapenzi, mambo ya kujua moyo wa mwenzangu sio matatizo as long sijaona moyo wake...Na siamini kama moyo wa binadamu unaweza ku ujua kuliko anavyo ujua mungu... lakini pale pale kuna sababu ambazo zinafanya mtu ajiamini kuwa aliye naye anampenda :first:

...hata sisi tulioumizwa tulikuwa na maconfidence kama wewe,hatujaumizwa na strangers !tumeumizwa na tuliowapenda na kuwaamini..tuliokuwa tumewaweka kwenye mioyo yetu...
Wanasema kila mtu ana bahati yake, we kama ulio wapenda walikumiza sio wote tunao wapenda watakujatumiza...Ulio wapenda wewe sio nilo wapenda mimi :A S-coffee:


......sikuombei mabaya
Hata ukiniombea mabaya hayata nifikia, sababu sio kila unacho kiomba wewe kizuri au kibaya takipata...siri anaijua mungu kwanini kuna badhi ya maombi hayatokei, lakini nashukuru kama hunombei mabaya :biggrin1:

but sipendi the way unavopondaponda vitu humu....
Kama nimekuponda nisamehe, si unajua sisi binadamu wote tunakasoro zetu :A S shade:


.....love u
I love you too :biggrin:
 
Sio kama sijakuamini, I'm just implying that uko very vulnerable na kuambukizwa, sio hiv tu. Na kama vidonda vyako haviponi haraka inakuweka kwenye hatari ya kupata tetanus pia. Mtu ambae hayuko vulnerable kama mimi anahitaji kujikinga wakati tu wa kuhudumia mgonjwa. Lakini kwa wewe uwe muangalifu wakati wote hata ukiwa karibu na watu ambao hujui status zao.
king´asti hapo pekundu panaonesha kabisa kuwa hujaamini nilichosema.
ngozi yangu ni ya kawaida tu mpendwa wangu ila ukweli ndio huo,tena paliweka hadi kidonda kilichochukua siku kadhaa kupona.
Mim nampenda mama mkubwa wangu,siwezi kumnyanyapaa yeye wala mtu yeyote hasa sasa hivi baada ya kupitia haya.
Asante kwa pole.
 
Last edited by a moderator:
Ukimwi & cancer.........haya magonjwa yanatisha jamani!!

BTW; hofu ni mbaya jamani, unaweza jikuta unaugua kitu ambacho hata hukukitegemea
Pole queenkami!
 
Last edited by a moderator:
story yako na mimi imeshanikuta.mwanamme wangu wa kwanza,baada ya muda tukaachana.jamaa mwenyewe alikuwa hajatulia.baada ya kuachana,kuna mtu alimuona akaniambia amepungua,mimi moja kwa moja nikachukulia ameathirika,hata kumuona sikumuona.na mimi nikasema kimoyo moyo ninao,nikawa sina raha,na nikawa naumwa mara kwa mara kwa ile hofu tu.nikasema mbona sina bahati,mwanamme wangu wa kwanza katika maisha yangu amenipa huu ugonjwa.siku niliojikokota kwenda kupinda,niliharisha hatari.wakati nasubiri majibu,nilijua tayari majibu ni positive.sikuamini nilivyoambiwa ni negative,magonjwa yote yaliisha,it was 12 years ago.nchi niliyokuwepo nilifanya full medical check up again,kila kitu ok.ila somo nililopata i really respect mtu ambae ni hiv positive,stress za mwanzo mwanzo hizo wanazozipitia,mimi nimeshazipitia.na tatizo la huu ugonjwa,upate support maana kuna wengine wanakuhesabia kabisa miaka,na wanakuambia pole mbele yako,ila pembeni story huwa ni tofauti
 
na huyo x wangu,baada ya kama miaka 7 nilikuja kumuona kwenye harusi,sikumficha nikamuelezea,akaniambia alishawahi kupima,na ni negative,kwa sasa ameoa na ana watoto 2,na mswalihina kama yeye hakuna tena.uhuni wote ameuacha
 
Mungu atulinde. Huu ugonja Mungu katuadhibu vibaya sana. In any way kuukwepa ni vigumu sana especially kwa watu walioko kwenye mahusiano.
Mwokozi tutoe tuepushe na hili balaa
 
nikajitafutie presha ya nini wakati siumwi?

Haya ndo mambo ya kuamsha mashetani yalolala. Aku!

mimi nilipima na aliekuwa mpenzi wangu kwa kulazimishwa sana..even tho alinitosa ila huwa naona aliniokoa kwa mengi ....
 
“BWANA, atawapigania ninyi na ninyi mtakuwa kimya katika amani”
Maneno haya ya Musa yanatupatia somo muhimu sana, Mungu huokoa.Ni wajibu wetu kuamini na kutii. Tunaona
jinsi Mungu alivyomwezesha Musa kuwa mkombozi; jinsi Mungu alivyowapatia wana wa Israeli njia ya wokovu,
wakati malaika wa mauti alipopita na tunaona jinsi Mungu alivyoifungua bahari ya Shamu ili kuwaokoa wana wa
Israeli na wakati huo kuwaangamiza wamisri
“Kwa imani wakapita kati ya bahari ya shamu kama katika nchi
kavu”
(Waebr 11:29)
 
Pole sana QK,maana naelewa hali uliyoipitia kwan ilishanikuta miaka 3 iliyopita,
Kuna binam yetu alipatwa na huu ugonjwa na akaficha hakusema wala hakutaka kutumia dawa mpaka alipozidiwa familia ikamfukuza akaja kwangu nikampokea na kuanza kuuguza nilikua nafata maelekezo ya DR namna ya kumcare but kikweli kuna wakati alikua inatokea aither ametapika gafla mda wa kutafuta gloves mpaka uvae hamna nahudumua ivo ivo nakumwomba mungu tu,

Baadhi ya ndugu wakanihesabia kbs eti nishaathirika kwa vile ninavomhudumia mara kadhaa mameno yale yalinitia hofu nakujihisi kweli nishaambukizwa,na wakati mwingine nilikua naharisha kbs,napata homa mpaka vidonda vinatokea mdomon but Dr akanambia ni hofu na kweli ilikua hofu na sikupata tatizo lolote!

Mungu ni mwema vidonge vikamsaidia na CD4 zikaongezeka akapata nafuu na kupona magonjwa yote nyemelezi afya imeimarika na akarudi kwake na akapata kazi na ni mrembo hasa na anaendelea na maisha yake akitumia dawa,nami nikabaki na amani tele huku nikifarijika kwa kumsaidia wakati wa uhitaji wake,

But kikweli huu ugonjwa haukwepeki hata kidogo as long as tunaishi na binadamu wenzetu,na kamwe ambaye hajauguza au kupata shuhuda za watu,ni ngumu kuelewa na kujua namna kunyanyapaa kunavoumiza!

Tuomembe tu mungu atusaidie na kutupa umri mrefu no matter tunao au hatuna.
 
Mungu atulinde. Huu ugonja Mungu katuadhibu vibaya sana. In any way kuukwepa ni vigumu sana especially kwa watu walioko kwenye mahusiano.
Mwokozi tutoe tuepushe na hili balaa
Kimweli uko kwenye mahusiano halali?namaanisha ndoa? kama ndio liko tumaini..wapo wanandoa ambaye mmoja wao alikuwa + wakati mwenzie ni - ....ni kwanini ni sababu achimbae shimo atatumbukia mwenyewe. ila its not automatic unapaswa kuwajibika ombea ulinzi ndoa yako na familia nzima ,tumia damu ya Yesu kuondoa tamaa zote za kiwili ambazo mara nyingi ndizo hasa chanzo...sasa mwenzio akiukwaa huko....u wont be responsible kabisa na ukimwi wenyewe utakuogopa kwa maana ulinzi umekufunika na kukuzingira.
 
Back
Top Bottom