Mkuu wangu
funguo kwanza kabisa kama kweli umeathirika nashukuru maana unajua kuwa kuwa kuwa na HIV sio mwisho wa maisha,na hiyo ni spirit nzuri na Mungu azidi kukupigania,sikupi pole maana nitakua kama nakuvunja moyo na kukufanya ujisikie vibaya.
Ila mkuu nimejifunza kuwa hapa JF mtu akiamua kupinga chochote ulichoandika hatakosa cha kukosoa na kukupinga,kama wewe,hapo kati unaniambia TUMSHUKURU MUNGU KWA KILA JAMBO,kule juu nimemshukuru Mungu kwa kuniepusha na balaa kwa kusema Mungu ni mwema kwangu umekasirika,sasa hata ningeandikaje nadhani ungekosoa tu maana humu kuna watu wao wako makini kutafuta kitu cha kukosoa tu.
Hapo pa zambarau ndio yale yale ninayosema wewe lengo lako lilikua kunikosoa tu,faida unazozipata kwa kufanya hivyo unazijua mwenyewe,anayejiona bora angeacha kitanda cha hoteli akalale chini?Anayejiona bora kwa kuwa yuko negative angeenda kulala na kula nyumbani kwa mtu anayejua kabisa kuwa ni muathirika?Hapa naona umenihukumu.
Mwisho wa yote nakutakia kila la kheri na pia Mungu ni mwema kwako pia,angekuwa si mwema kwako sidhani kama leo hii ungekua na nguvu za kuperuzi pamoja nasi hapa JF.Ubarikiwe.