Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...


Pole kwa hofu jouneGwalo.

Sasa wewe kichwa cha habari tu kinakutia hofu pata picha mimi ilikuaje wakati sina uhakika kuwa ni neg au positive.
Ni wakati mgumu asikwambie mtu,sasa naelewa umuhimu wa watoa ushauri nasaha maana kama hauko jasiri huwezi kwenda kupima kitu ambacho kinazidi mateso ya kisaikolojia.
UKIMWI umechukua taji la kutisha japo kuna magonjwa mengine yanatisha zaidi kama cancer na mengineyo ila ukimwi ni habari nyingine jamani.Mungu atuondolee hili janga jamani linatisha.
 
Last edited by a moderator:
Mpaka mwili umeni sisimka! Pole sana QK..
Be careful na huyo aunt yako. Watu wengine hawachelewi kukuchana na viwembe kusudi akuhamishie gonjwa.. Dunia hii jamani!
 

Pole sana mamie,
Dah, umenikumbusha miaka ya nyuma niliwahi kuugua hofu ya kuwa nimeathirika. kiukweli nilipungua uzito niliwaza sana. basi kulikuwa na doctor mmoja hivi rafiki yangu, nikamfuata nikamweleza kuwa ninaumwa, basi akaniuliza naumwa nini? nikamwambia naumwa hofu ila naogopa kupima. kama mjuavyo madakrati wana mbinu nyingi za kuwashauri wagonjwa wao, basi akanambia mimi nitakupima malaria, typhoid, VDRL na magonjwa mengine yote ila HIV sitakupima mpaka utakapoamua mwenyewe. basi c nikatoa damu kwa hiyari ili kupima kwanza magonjwa mengine....... Lahaula, kumbe yeye alikwenda kupima na HIV bila KUNAMBIA. alivyomaliza kupima hivyo vipimo vingine akanambia kuwa hauna magonjwa yoyote yale na pia HIV status yako ni NEGATIVE. nilifurahi sana na kujiona nimezaliwa upya.... baada ya muda nikaenda tena kucheck kwenye hosp. nyinge pia majibu yakawa NEGATIVE. Ushauri unaweza ukawa na hofu ukaugua ugua kumbe huna HIV ila ni magonjwa ya kawaida tu hata kama ungekuwa huna HIV ungeugua lakini kwa sababu una hofu utafikiri kuwa umeshaathirika. ni vymea kujua status yako mapema kuliko kubaki na assumption...........
 

Woow nimeipenda mbinu ya huyo daktari.
Amekusaidia sana maana kama sio hivyo ungeendelea kuugua ukimwi wa kuhisi.
Ila angekuta Positive nadhani asingekwambia,ila negative ni habari njema.
Ila ukiambiwa huna unajiona tajiri si tajiri,yaani ni raha tupu.
Pole kwa hofu uliyopata charminglady.
 
Last edited by a moderator:
pole sana..............ILA MI LAZIMA NITAJITENDA NA WAGONJWA WA UKIMWI,NITAWANYANYAPAA
 
pole na hayo ndio maisha kihoro ndio kinaua watu wengi tupimeni tujue afya zetu na tutaishi kwa amani sana
 
Pole sana kwa mawazo, mawazo ya aina hiyo yalishamfanya ndugu yangu mmoja aumwe mpaka basi, kisa shugamami lake la siri lilikufa na ngoma watu walikuwa wanasema but yeye kumbe alikuwa safi kabisa, na umalaya alipunguza vibaya mno, kuna waathirika ambao mawazo ndio yanayozidi kuwadhoofisha zaidi kuliko hata unyanyapaa, just mtu anatakiwa kuchukulia poa, kula balance diet na kurefresh mind yake kwa vitu ambavyo ni fun, or ni hobbies zake, but asifanye mazoezi magumu sana, yatamchosha mno
 
siku hizi hakuna kupima tena, ukimwi haupo ndugu zangu,
 

1. Mtu haambukizwi ukimwi. Anaambukizwa virusi. Jifunze tofauti ya HIV na AIDS.
2. Ukipima kuna aina tatu za majibu: una virusi, huna au "hali ya isiyotoa hakika ya yoyote kati ya hayo'.Pima zaidi ya mara moja ikiwezekana kwa vipimo tofauti.
3. Acha unyanyapaa wa maneno na vitendo.

BTW: nini lengo la hii post yako?
 
hii inanikumbusha stor moja ya nyoka, kunguru na binadam...nyoka alikuwa anabishana na kunguru kwamba mara nyngi kinachomuua bnadam ni HOFU na sio kingne. Ubish ulkuwa mkubwa ikabid wafanye zoez moja kuhakikisha, ikawa hivi...nyoka na kunguru wakajfcha kwenye majan bnadam alpopta nyoka akamgonga bnadam kwenye mguu halaf akajfcha, kunguru akatoka kwa kelele, bnadam alpomwona ni kunguru hofu ikaisha akaendelea na safar...wakarudia zoez lao kwa kubadlshana, wakati huu kunguru akamgonga bnadam mguuni, akajfcha, nyoka akatoka akikimbia eneo lile na bnadam akamuona kilichofata nadhan jibu unalo...pole sana Qk
 
Poleni sana kwa hayo majaribu ila naamini mungu aliwapigania kwa sabu ya nia yenu njema.
Mimi nahisi kwa maisha ya sasa mtu kujua status yake ni jambo la msingi sana...
 
Hichi kitu babu aliniambia kuwa imani huleta ugonjwa ila sikuamini ila leo nimeamini kwa mfano huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…