Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

Sikutegemea kama ingetokea siku na mimi nijihisi nimeambukizwa UKIMWI...

Bado ulikosea sana, unaishi wka sandakalawe.......na wasomi wengi sana wana matatizo HAWAJUI ukimwi, ila wanadhania wanaujua!!

ulichotakiwa kufanya

1. Nenda hospitali haraka within 72 hours upate kinga, hii ina itwa PEP-post exposure prophylaxis ! hakuna cha kusali wala cha nini

Vijidudu vya HIV huchukua masaa 72 kuingia kwenye cell ambako vitaishi siku zote, ukiweza kuvizuia visifike huko basi wewe mzima PEP inafanyanya hivyo

Kwa watoto wa mjini Septrin inatumika kama PEP!!! ha ha ha

Mkuu ni kweli ilinipasa kufanya hivyo ila wakati huo sikuwa najua mambo ya PEP.
Nashauri mkapime tena ukizingatia kwamba kuna vipimo vya VVU havikufikia viwango vya TBS ndio maana hata matokeo ya Samunge yalikuwa tata (msitishike lakini)!
.

Mkuu Companero nilipima nje ya nchi wana teknolojia za hali ya juu.
Pia nilipima ikiwa zaidi ya miezi minne ishapita.
Pia umesema unashauri "mkapime",hapo sijakuelewa unashauri mimi na nani tukapime?
 
Last edited by a moderator:
mwenzako naye amepima? na window/incubation period ilipita?

Mwenzangu yupi? unamuongelea FirstLady1 au?

Sasa mkuu Companero incubation period si inawahusu watu ambao tayari wameathirika.
Mimi ninavyojua incubation period ni hatua ya kwanza ya ugonjwa wa HIV ambapo mashambulizi ya virus vya ukimwi huanza kuonesha dalili.
Hata hivyo mtu huwezi kujua kama incubation period imepita au la mpaka hapo utakapoanza kuona hizo dalili kama wewe ni muathirika kwa sababu inatofautiana kwa mtu na mtu.Kuna watu wanaanza ona dalili baada ya wiki mbili baada ya maambukizi na wengine inaweza kuchukua hata miaka kumi ndio dalili zionekane.Watu wenye genes zenye nguvu huwachukua muda mrefu kushambuliwa wenye weak genes ndio hivyo huona dalili mapema.
 
Last edited by a moderator:
Dah queenkami pole sana ..
Mie nakumbuka rafiki yangu alikuwa anaumwa sana ila hakunambia nini kinamsumbua ingawa siku zote alinihakikishia ana vidonda vya tumbo..
Kwa sababu nilikuwa naamini ni rafiki yangu mpenzi na ni mtu niliyemwamini siku zote,..
Nilikuwa namuuguza kila anapoumwa ..kuna kipindi alikuwa anafikia hali ya kutokuweza kuamka kitandani namuogesha na kumlisha..
Nilipatwa Presha siku Dr aliponiuliza madame hivi huyu Best friend wako ukimuogesha huwa unatumia Gloves
Nikamuuliza Why ndo akanifungia ofisini kwake na kunipa habari kamili..
Mwili ulinyong'onyea
Jasho lilianza kunitoka
Na kuhisi kizunguzungu..
Nilikuwa na hali ngumu sana....
Ila mungu ni mwema siku zote..

FirstLady1, mie nilifikiri ma first lady kila kitu mnafanyiwa, sasa huyo alikuwa ni rafiki tu au rafiiiki?
 
sweetlady asante dear. chukualia mfano unaambukizwa kwa style kama hii yangu halafu unajifanya mcha Mungu hivi ukiwaambia watu kuwa sijaupatia kwenye zinaa watakuelewa kweli?au si ndio utaonekana chui kwenye ngozi ya kondoo..Mimi mpaka naamua kwenda kupima mawazo yangu kwa asilimia kubwa yalishawishika kuwa ninao hivyo nikaona bora nikapime ili kama ni dozi nianze mapema kabla sijaanza kutokwa na mapele na kukonda hadi watu wakaanza kunishangaa.Mpendwa wangu ukiwa katika hali hii ya kujihisi unao ni mateso yaani tumuombeni Mungu atuepushe.
Oooh!!!!@queenkami my dearest yaani ni kuomba sana Mungu atuepushe na majaribu ya dunia, kiukweli hakuna atakayekuelewa......dunia ya sasa watu tumezoea kusema hata vile tusivyovijua undani wake......hivi unadhani ni kwanini walioathirika wengi huwa wanaogopa kujitangaza???......wengi wao huwa wanaogopa maneno ya watu.....maneno yanakondesha, yanakosesha amani na wakati mwingine yanaua upesi kuliko hata ugonjwa wenyewe........hivyo kuliko kujitangaza mtu anaona nafuu kukaa kimya... pole mpendwa kwa kukumbwa na majaribu.....wakati mwingine ni vema kumshukuru Mungu kwa kila jambo....kumtanguliza Mungu kwenye kila jambo tulifanyalo katika maisha yetu nalo ni jambo la busara manake kiukweli dunia ni kubwa na peke yetu kamwe hatuwezi kufika!!!!
 
Last edited by a moderator:
Dah queenkami pole sana ..
Mie nakumbuka rafiki yangu alikuwa anaumwa sana ila hakunambia nini kinamsumbua ingawa siku zote alinihakikishia ana vidonda vya tumbo..
Kwa sababu nilikuwa naamini ni rafiki yangu mpenzi na ni mtu niliyemwamini siku zote,..
Nilikuwa namuuguza kila anapoumwa ..kuna kipindi alikuwa anafikia hali ya kutokuweza kuamka kitandani namuogesha na kumlisha..
Nilipatwa Presha siku Dr aliponiuliza madame hivi huyu Best friend wako ukimuogesha huwa unatumia Gloves
Nikamuuliza Why ndo akanifungia ofisini kwake na kunipa habari kamili..
Mwili ulinyong'onyea
Jasho lilianza kunitoka
Na kuhisi kizunguzungu..
Nilikuwa na hali ngumu sana....
Ila mungu ni mwema siku zote..

pole sana FL and QK maisha yana changamoto nyimgi and that is party of it be carefully UKIMWI upo na unaua
 
Pole sana, hiyo hali uliyopitia ni ngumu sana na inaweza kukuletea presha na magonjwa mengine. Nasema pole tena kwani nilishapitia kwenye hali kama hiyo.Nakupongeza sana kwa hatua uliyochukua ya kwenda kupima. Mpaka sasa kuna watu wanaishi kwa hofu, hiyo ni mbaya na unaweza kufa tena ikitokea mtu akasema aah umekonda unachanganyikiwa kumbe kukonda kunasababishwa na mawazo uliyonayo.Jamani tupime afya zetu hii inakufanya uishi kwa amani na kupanga mipango yako. Km umeathirika inakusaidia kupanga lishe ili uweze kuimarisha kinga ya mwili pia unapanga mipango mingine ya maisha.Mshauri mama yako mkubwa aende tena kituo cha ushauri nasaha ili aweze kupata dawa ambazo zitamkinga na magonjwa nyemelezi. Kukataa kutumia dawa inawezekana ni kwa sababu amekata tamaa. Nakuomba umsaidie hata upande wa lishe kwani anahitaji lishe nzuri.
 
FirstLady1, mie nilifikiri ma first lady kila kitu mnafanyiwa, sasa huyo alikuwa ni rafiki tu au rafiiiki?

Rafiki yangu wa Kike bana niliye mchukulia kama ndugu wa damu nilimpenda na akanipenda na hata pengo lake hapa duniani halijazibika mpaka leo..so ilikuwa wajibu wangu kumsaidia...
 
Duh. . .poleni sana Mama wa kwanza na QK. . .
Watu wengine hua wakishaupata hawajali ikiwa wataambukiza wengine au la. Pengine mama mdogo wa QK alimkata kwa makusudi kabisa.

Da Lizzy,
Ni kweli kabisa wapo watu wanaoambukiza wenzao kwa makusudi. Kuna familia moja DAR walimchukua ndugu wa mwanamume toka huko mikoani aliyekuwa mwathirika kwa ajili ya kumhudumia kwa karibu zaidi lakini yule mwathirika alikuwa ni "shetani". Ilifika kipindi watoto wawili wa familia hii walianza kuumwa bila kukoma na walipowapima damu wakaonekana kuwa wameathirika. Daktari akaumuuliza baba wa watoto je una mgonjwa wa ukimwi nyumbani kwako baba watoto akasema ndiyo. Ikabidi wafanye utafiti humo ndani na kuja kugundua kuwa yule mgonjwa akiingia bafuni anajisukutua kwa kutumia miswaki ya wale watoto na kuacha damu pale na watoto bila kujua wanakuja kuitumia ile miswaki na ndo chanzo cha kuambukizwa. Kwahiyo ndugu zangu yapasa kuchukua tahadhari kubwa ukiwa na rafiki au ndugu anayeumwa huo ungonjwa. Nyumbani kwako kama una watu wengi hakikisha miswaki yako na ya watoto wako haibaki bafuni n.k n.k.

NB: Hata kwenye shughuli zako e.g biashara kuwa makini na rafiki zako maana wiki iliyopita mtu mmoja huko Kongowe (Kibaha) amepigwa risasi kwenye taya na rafiki zake wawili wa karibu kunyang'anywa VX, dola 30,000 na pesa za Ki-TZ na vitu vingi vyote kwa ujumla vikiwa na thamani ya Tshs. mil. 310.
 
wabongo pia tuache tabia za kuzushiana ngoma..kitaa kilinika pale walipomzushia deme flani kafa na ngoma wakati yupo hai..noma sana..
 
usimwamini mgonjwa wa ukimwç hatakama ni mama yako unapaswa kuwa makini sana maana huu ugonjwa wakati mwingine ni pepo
 
Aaagh.....!
Yaani we Qk ni msanii, title ya thread ilinifanya niogope kuisoma toka nlipoiona mara ya kwanza!
Leo nipo eneo hapa nimeona ngoja nijitose kuisoma, basi nimeisoma roho ipo juu juu tu hadi kufika mwisho ndo nimepumua lol,
so kumbe mtoto hujaathirika!
Haya furaha iwe nawe, ila duu umepitia wakati mgumu sana kiakili,
kwa kweli i can imagine what u ve been thru!
 
Pole sana, hiyo hali uliyopitia ni ngumu sana na inaweza kukuletea presha na magonjwa mengine. Nasema pole tena kwani nilishapitia kwenye hali kama hiyo.Nakupongeza sana kwa hatua uliyochukua ya kwenda kupima. Mpaka sasa kuna watu wanaishi kwa hofu, hiyo ni mbaya na unaweza kufa tena ikitokea mtu akasema aah umekonda unachanganyikiwa kumbe kukonda kunasababishwa na mawazo uliyonayo.Jamani tupime afya zetu hii inakufanya uishi kwa amani na kupanga mipango yako. Km umeathirika inakusaidia kupanga lishe ili uweze kuimarisha kinga ya mwili pia unapanga mipango mingine ya maisha.Mshauri mama yako mkubwa aende tena kituo cha ushauri nasaha ili aweze kupata dawa ambazo zitamkinga na magonjwa nyemelezi. Kukataa kutumia dawa inawezekana ni kwa sababu amekata tamaa. Nakuomba umsaidie hata upande wa lishe kwani anahitaji lishe nzuri.

Okay mkuu nitaendelea kujitahidi apate hizo huduma Honest1.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom