Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Niliozesha pacha wangu kama miaka mitano ilishapita ,huko kwa wahaya nilihakikisha anaenda bure kabisa kwa sababu wajomba walitaka kuingiza drama ila sisi kama familia hatukua tunataka chochote ,kwa sababu mahari ni kama biashara tu.
Kwani kwenye mahari wajomba lazima wawepo
 
🤣🤣🤣 Hayo maamuzi ya Kiume sanaa . Unajua kuoa una unganisha udugu, watu wanafanya kama mnauziana binti ,mna komoana then kesho yake bado watakuja na kuombana sijui mjomba hivi, baba vile au naend home kuuguza.

Mahari ni zawadi tu, Sio chanzo cha mapato wala mtaji kwa wazeee.
 
Usiogope! Unachopaswa kufanya ni kutoa ulichonacho hata kama umeambiwa ni shiling ngapi! Mahari haiishi kulipa.
Mkuuu! Kuna familia za ovyo sanaaa. Unaweza kujikutana masimango kisa hukumaliza mahari, au watu wanaanza kufanya maamuzi ya chini chini kukunyima sauti kisa hujamaliza mahari...
 
Ukiona wanakupandishia mahari kwa kudhani una pesa ya mchezo, waambie ngoja nikazitafute halafu block simu zao zote hata simu ya huyo binti Yao, then endelea na ustaarabu mwingine. Binti mwenyewe labda ana ma X kibao na wazee wake wanajua Ila tu kwa kuwa umekua muungwana umekwenda kujitambulisha wanakuona bwege.
 
MTIE MIMBA halafu kausha, hudumia mimba azae akiwa kwao, hudumia mtoto,
Ukiona kimya MTIE MIMBA nyingine hudumia kama kawaida,
wakileta jeuri TIA MIMBA nyingine, watamleta kwako wao wenyewe tena na gharama za usafiri ni juu yao.
Unamwingiza chaka mwenzio mchana kweupe! Atashushiwa mshipa wa ngiri mpaka akome! Yaani kazee kanamhesabu binti kama mtaji uje ukachafulie katakuacha salama? Kikubwa afanye negotiation vizuri tu mbona dingi atashuka! Hapo 2m uhakika!
 
Naomba namba ya huyo mchumba wako kuna kitu nataka nimuelekeze
 
Kujitoa kwako ukweni ndio sababu ya wao kukupiga parefu.
 
😁😁Mkuu chunga sana usimwamini sana binti yako, tusije kukukuta juu ya mwembe

Parapanda mara nyingi huanza hivi.

Trust - disappointment - BP+stroke+heart attack/suicide, then history.
 
😁😁Mkuu chunga sana usimwamini sana binti yako, tusije kukutungua juu ya mwembe.
Ukiona binti ana mambo ya ovyo ukweli ni kuwa umefeli kama mzazi. Na kufeli kupo sikatai, akiwa binti wa hovyo anayeshindwa kuniheshimisha she ain't my daughter
 
Unamwingiza chaka mwenzio mchana kweupe! Atashushiwa mshipa wa ngiri mpaka akome! Yaani kazee kanamhesabu binti kama mtaji uje ukachafulie katakuacha salama? Kikubwa afanye negotiation vizuri tu mbona dingi atashuka! Hapo 2m uhakika!
Milioni 2 ananunua ng'ombe wa maziwa au.. Halafu masuala ya mzai kutaja mahari utafikiri ye ndio muolewaji, utaratibu huo haufai, mahari ni zawadi ya binti muolewaji toka kwa mume.

Kwa mujibu wa imani ya dini yangu,
Kwamba nimeenda kuposa, binti kanikubali, kule kunikubali mimi, yaani huenda kaishakataa wengine huko, hivyo kwa furaha ni kumuuliza nikuoe zawadi gani, yeye ndio anataja, zawadi hiyo ndio inaitwa MAHARI.
 
Sasa mkuu mila unalinganisha na imani ya dini? Usukumani mahari ni ya baba! Ndiyo maana huwa kuna utaratibu wa kwenda "kuloma mpango!" Mzee anachagua wazee wenzake wanaenda ku-bargain mahari! Siku moja nikasakiziwa vijana wa Kiha kwenda kuwatetea kwenye mahari vizee vya Kisukuma vikang'ang'ania 5m, vijana wa Kiha wakakata tamaa ya kupata binti wa Kisukuma! Mwisho wa siku tukayamaliza pamoja na vutankuvute!
 
Aiseee........ nadhani ulikosea kuwaambia waondoke,wangerudi na kuwaambia basi sisi tunaondoka,tutarudi tukiwa tayari.
 
Tafuta hiyo milioni 6 nenda Karatu au Manyara kakodi shamba la milioni 3, hiyo 3 nyingine ifanyie mipango ya kulima. Muda wa kuanza kuandaa mashamba unakaribia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…