Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Uislamu raha sana kwenye jambo kuoa moja mahari ni ya mwanamke yeye ndio anataja anataka nini kama seti ya sahani sawa kama mkeka wa kuswalia sawa ... Jambo la kuzika na jambo la kuoa limefanywa rahisi na la haraka mno .
Pole mkuu lipa hiyo mahari mambo ya mila ya ajabu ajabu waachie wenyewe
Hii ni kwa waislam maskini, nenda kwa GSM au Mo na hizo sahani zako tuone matokeo yake
 
Kwa sasa mahari + kila kitu visizidi 1.5m, zaidi ya hapo ni kubebesha vijana mizigo isiyo na maana.

Hata hivyo mimi huwa napingana sana na mahari kwa sasa, mabinti wengi walishaharibiwa, hawana bikira, walishazalishwa, wengine hadi kinyume wanaenda, hawana adabu na hata utulivu wao ni zero kwenye ndoa, sasa mahari ya nini.
 
Wachaga hawajawahi kubwa na mahari kubwa ndio kabila moja wapo lenye mahari ndogo , ukitoa vitu kama vitenge vya bibi ,shangazi na debe la mbege unachukua msalaba wako.
Mmmh, mkuu tuliooa uchagani tuna testimony aisee. Ile cash ya mahari inaweza isiwe kubwa sana, ila makorokoro ni mengi sana, unaweza kutajiwa cash ya 1m, ila ukiweka na mambo mengine hata 3m inafika.
 
Wakuu habari za muda huu
Kijana wenu nina umri wa miaka 28
Baada ya kuona kwamba sasa yanifaa kuwa na mwenzangu wa kuishi nae basi nikachukua jukumu la kwenda kwao kujitambulisha na kufahamika rasmi ili basi niishi nae kihalali kabsa
Kipato changu sio kikubwa sana hvo nikawa nimejiwekea kias flan kama mahari (million 1) nikamwambia mwenzangu kwamba hima hima kaongee na mama kama ataweza kuongea na mzee bc mahari isizidi hapo.

Mwenzang akanifata na kunijulisha kwamba mzee amekubal lkn anaomba angalau basi iwe 1.5 ili waweze kugawana nyumban na baadhi ya ndugu kwakuwa natambua kwamba mahari huwa haiishi (baada ya kuelezwa na wakubwa wangu) bc nilikubali kulipa hyo 1.5 lkn kwa malipo ya kidogo kidogom

Jana kwa neema ya Mungu ndugu na familia yangu wakaongozana hadi kwao na mwenzang kwa ajili ya kutoa kishika uchumba na pia kulipa nusu ya mahali tuliyokubaliana
Baada ya kufika huko ndugu zangu hawakuamin walichokutana nacho huko ambacho ht mm mpk sasa siamin bado.

Mahari wamekuta ni million 4 na mahitaji kama koti la babu na vitu vingine jumla million 2 yan TOTAL ni million 6.

Kwa bahati mbaya sikuwepo ila laiti kama ningekuwepo bc ningewaomba ndugu zangu turudi nyumban
Nimesikitishwa sana na kilichotokea jana japo ndugu wamenishauri nisioneshe nia ya kukataa kuendelea na binti huyo lakini naona kabisa sitoweza najiona nikimuacha na kuendelea na maisha yangu
Ukweni wamenionesha rangi halisi kwamba kwao pesa ndio kipaumbele kikubwa kulko upendo.

Roho imeniuma sana nimejitoa vitu vingi sana ukweni kabla ya cku ya jana malipo yake ni mahari ya kukomoana kiasi hiki

Wakuu naombeni faraja zenu na ushauri wenu nifanye nini katika swala hili.

Natanguliza shukran🙏
kwanza uelewe kwa tamaduni nyingi mahari inaongelewa na ndugu/ukoo na si baba wa binti tu
kwahiyo hao watu ndo wanatakiwa kushawishiwa kwamba uwezo wako ni huo wa 1.5
huku tarime sisi tunaolea hadi ng'ombe 20 na 30 hiyo ni kama M10 hadi M20
 
Back
Top Bottom