Kuna siku tulikwenda kumuwakilisha dogo kwenye kutoa mahari, Kuna kiasi elekezi tulichoambiwa, kufika ukweni kabla ya kula tukaingia kufanya negotiations kwanza. Wakwe wakatuona labda tuna pesa Sana wakapandisha kila kitu zaidi ya Mara nne kupunguza wamegoma. Sisi tukasema hebu tutoke nje tukatete halafu tunarudi kutoa mrejesho. Ile kutoka nje tukampigia muoaji simu kwamba Mambo huku si Mambo. Dogo akasema, Wala msirudi kuaga ingieni kwenye gari rudini acha wale chakula Chao wenyewe na Mimi nambwaga binti Yao. Kwani tutakutana nao wapi sisi kila mtu anatokea mkoa wake. Ndio ikawa binti arudi sokoni Tena kutafuta mchumba mwingine.