Sikutegemea nilichokikuta ukweni

Hii ni kwa waislam maskini, nenda kwa GSM au Mo na hizo sahani zako tuone matokeo yake
 
Kwa sasa mahari + kila kitu visizidi 1.5m, zaidi ya hapo ni kubebesha vijana mizigo isiyo na maana.

Hata hivyo mimi huwa napingana sana na mahari kwa sasa, mabinti wengi walishaharibiwa, hawana bikira, walishazalishwa, wengine hadi kinyume wanaenda, hawana adabu na hata utulivu wao ni zero kwenye ndoa, sasa mahari ya nini.
 
Wachaga hawajawahi kubwa na mahari kubwa ndio kabila moja wapo lenye mahari ndogo , ukitoa vitu kama vitenge vya bibi ,shangazi na debe la mbege unachukua msalaba wako.
Mmmh, mkuu tuliooa uchagani tuna testimony aisee. Ile cash ya mahari inaweza isiwe kubwa sana, ila makorokoro ni mengi sana, unaweza kutajiwa cash ya 1m, ila ukiweka na mambo mengine hata 3m inafika.
 
kwanza uelewe kwa tamaduni nyingi mahari inaongelewa na ndugu/ukoo na si baba wa binti tu
kwahiyo hao watu ndo wanatakiwa kushawishiwa kwamba uwezo wako ni huo wa 1.5
huku tarime sisi tunaolea hadi ng'ombe 20 na 30 hiyo ni kama M10 hadi M20
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…