Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada kuu.
Mimi hapa nimezaliwa mjini Daslamu miaka mingi nyuma kabla ya mwaka 2000, kwa mazingira niliyokulia na watu wengi tulioishi nao ni Wazarumu. Lakini cha kushangaza sikuwahi kuona Mzaramu Mkirstu wengi tulioishi nao mpaka leo ni Waislamu, hii ikanipelekea kujua kwamba hakuna Mzaramu Mkristu.
Sasa cha kushangaza Jana katika pitapita zangu za huku na kule nikakumbana na Bidada mmoja hivi mrembo amenyooka nikamuelewa tukaanza maongezi ya hapa na pale kuchombezana tulipofika kwenye kujua yeye kabila gani akasema Mzaramu ila ukimuangalia ni km Mchagga wa Marangu maana meno yameliwa na kutu, nikashtuka nilipouliza dini ndio nikashtuka zaidi akasema yeye ni Mkristu.
Hivi weewe pia ulikua km mimi ukiamini kwamba hakuna Wazaramu Wakristu yaan Wazaramu wote ni Waislamu?
Kwarezima njema wakuu.
Msiache kufunga na kwenda kupakaa majivu.