Sikuwahi kujua kama kuna Wazaramo ambao ni Wakristu

Mimi pia nilikutana na mdada mzaramo halisi ana miaka kama 18y ila ni mkristo ..nikamwambia wazaramo wakristo wametoka wapi ...tena mzaramo wa makanisani sana muda wote anawaza kwenda kanisani.
 
1. Kuna kubadili dini.
2. Kuna kuwa kwenye ukoo ambao huko nyuma mmoja alibadili dini, na waliofuata baada ya hapo wote wanaendelea na dini mpya
Ni kweli usemavyo Mkuu kama sisi kwetu huko Pwani walio wakristo wengi walibadili dini enzi hizo sababu ya kupata elimu.

Japo sasa kwa kuna baadhi ambao bado wanaishi vijijini wanavaa mashungi kama kawaida yaani utawatambua kwa majina tu.
 
Kwa hiyo wewe hata wapemba unadhani hakuna wakristo au hakuna wakristo mogadishu au unadhani hat pale macca na Madina hakuna wakristo?
Halafu wale wa Unguja, kuna lile kanisa la ST Joseph Zanzibar (minara miwili) karibu na posta ya kwanza Zenji, (nadhani yale maeneo ni stone town) wanaenda kusali wakiwa wamevaa kama wavaavyo waislamu
 
Mimi pia nilikutana na mdada mzaramo harisianamiaka kama 18 ila ni mkristo ..nikamwambia wazaramo wakristo wametoka wapi ...tena mzaramo wa makanisani sana muda wote anawaza kwrnda kanisani.
Hii imenishangaza sana Mzaramu Mkirstu ni nadra sana tena unahesabu mmoja mmoja
 
Wakuja ndio wanajenga Makanisa wewe unahisi Kisarawe na Pwani wanaishi Wazaramu peke yao hawawapokei wageni na kuwauzia ardhi na kujeenga makanisa yao?
Halooo uko uzaramuni wakatoliki ndo waliweka makazi miaka iyoo kuna majengo ya zamani unaambiwa apo ilikua ili usome lazima wakubadili dini ndo uandikishwe shule.
 
Halooo uko uzaramuni wakatoliki ndo waliweka makazi miaka iyoo kuna majengo ya zamani unaambiwa apo ilikua ili usome lazima wakubadili dini ndo uandikishwe shule.
Duuh hii ni mpya hii kumbe ndio ilivyokua?
 
Hii imenishangaza sana Mzaramu Mkirstu ni nadra sana tena unahesabu mmoja mmoja
Mimi mwenyewe nilishanga bora huyo wako amechanganya damu labda na wachaga nk ila mimi nimekutana na mzaramo halisi wa baba mzaramo na mama mzaramo ila ni mkisto ..ikabidi nimuulize kuwa sijawai kusikia mzaramo mkristo siku akija nitamuuliza vizuri imekuwaje ni mkristo
 
Mi sijawahi kuona mmasai muislam, nimeishi vijiji vya umasaini huko mikoa ya Arusha na Kilimanjaro naona ni wakristo tu wa madhehebu ya Kilutheri na Kipentekoste
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…