Sikuwahi kujua kuwa CCM inamiliki na Migodi

Sikuwahi kujua kuwa CCM inamiliki na Migodi

Kama kichwa cha uzi kinavyojieleza.

Sikuwahi kujua kuwa sisiemu inamiliki na Migodi.. Je kuna Migodi mingine ambayo Chama tawala kinamiliki?
Na huu Mgodi jina lake unaitwaje?

Angalia video hii inayomuonesha waziri Mkuu, Kasimu Majaliwa akitembelea mgodi wa makaa ya mawe uliopo Mdunduwalo, Wilaya ya Mbinga, Mkoani Ruvuma.

View attachment 2479419
ccm wanamiliki serikali utakuwa huo mgodi tena kipande tu
 
hizo V8 zote kwenye msafara bila shaka gharama ya mafuta tu hizo km za barabara zingekuwa tayari zimejengwa.
Mda ni mali kwa mda ambao CHADEMA mmeupoteza kwenye maandamano, makongamano, kususa na kuzira mngesha jenga makao makuu
 
Chama kinaweza kuwa na vitega uchumi kama majumba, nk.

Ila kwa ccm kumiliki mgodi!! hapa tumepigwa kabisa, maana mapato ya mgodi yanaenda kwenye chama sio kwenye mfuko wa hazina.

Hivi Kuna waziri anaweza aka muhoji mkurugenzi wa hiyo kampuni ya mgodi ya CCM?
Mkuu usiwe na hofu na nikutoe shaka CCM tunalipa kodi , tozo ,mrahaba, na leseni kwa kumiliki huo mgodi na malipo yote yanaenda hazina na CHADEMA mnapata ruzuku kutoka hapo
 
Huo mgodi watu wanejipigia mpaka wamevimbiwa na kutapika kabisa.. Mwaka jana walitaka kumuuzia tycoon mmoja ambaye alishawahi kushika wadhifa mkubwa kichama kwa BILLION 4 jamaa akawadengulia.. Sasa sijui wamepata wapi mtaji/mfadhili?
 
This is by all means not right?

Nchi haiendelei kumbe the ruling party owns everything... .. how are you going to compete kwenye market kama hii...

Na wafaidika wa gawio la miradi hii ni nani?

Kumbuka CCM ni Chama cha siasa kinachofaidika na kodi zetu kupitia ruzuku ikiwemo Michango ya wanachama bado wanazunguka kuomba michango kwa wafanyabiashara.

Country robbery... na hapo namuona wazir mkuu wanakwepa kabisa kuongea kwamba mgodi huu unamilikiwa na Chama Chake..

That's Bad, very bad
CCM is a legal person with all the right including the right to own property , sue and get sued. etc. ACHA CHUKI, ROHO MBAYA , NA AKILI MBOVU
 
Waliamua sehemu ya ruzuku na mapato mengine Kama ya viwanja na kuuza KADI,wawekeze..walifanya hili siku nyingi kipindi kile jakaya analalama wenye hela wanaowafadhili wanawasimanga
Hawezi kukumbuka walikuwa wanaandamana na kwenda kuomba hela ubalozi wa Ujerumani
 
Back
Top Bottom