PreGE2025 Silaha hii wanaitumia CCM dhidi ya upinzani na imewapa ushindi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020 na mwaka huu 2025 wanakwenda kuitumia tena

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Samia atosha tukutane2030

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
17,728
Reaction score
49,762
Sikumbuki tarehe ila ilikuwa kati ya mwezi wia 9 au wa 10 hivi 1995 nikiwa na miaka 8 hivi kwenye kitongoji chetu walikuja watu waliovaa nguo za kijani na njano wakitokea wilayani kuja kutuwekea muziki na kisha baadaye kuanza kuongea.

Wale watu nilikuja kuwakumbuka baadaye kidogo nilipokuwa . Ni viongozi wa CCM wilaya kwa ngazi tofauti.

Mama mmoja ambaye yuko hai mpaka sasa mweupe alipopewa mike kuongea alijifanya kuongea kwa uchungu sana kuwa watu wasipochagua CCM ikitokea vita watakaoteseka zaidi ni akina mama, watoto na wazee.

Hii silaha nimeona ikitumika kwenye kila kampeni.

Na upinzani umeshindwa kujibu ingawa majibu yake yalipaswa kuwa mepesi kabisa.

CCM ifike wakati muwahurumie wananchi.
 
watu wasipochagua CCM ikitokea vita watakaoteseka zaidi ni akina mama, watoto na wazee.
Kwa upande wa urais, uchaguzi uliishamalizika pale Dodoma ile January, kinachoendelea sasa ni mchakato wa kutimiza tuu kukamilisha taratibu na kusubiria siku ya siku tarehe ifike, mtu ni unakwenda tuu kituoni, kwa ajili ya
“unachukua...
unaweka...
....“
Malizia mwenyewe!
P
 
Class struggle itaamua, ccm hawez tawala milele, ogopa sana class struggle, mifumo mingi ya unyonyaj imeangushwa na class struggle, wanyonge wakishasema sasa inatosha, moto utawaka tu..!
Hata juzi kwenye baraza la Eid kiongozi alitoa kauli kana kwamba vyama vingine vikiingia Ikulu vitaleta vita
 
Kwa upande wa urais, uchaguzi uliishamalizika pale Dodoma ile January, kinachoendelea ni kutimiza tuu taratibu, kusubiria tarehe ifike,
Unakwenda kituoni
unachukua...
unaweka...
....
Malizia mwenyewe!
P
It's pathetic what hunger can do to one's mind but it is even more pathetic that this comment is coming from you.
 
Kwa upande wa urais, uchaguzi uliishamalizika pale Dodoma ile January, kinachoendelea ni kutimiza tuu taratibu, kusubiria tarehe ifike,
Unakwenda kituoni
unachukua...
unaweka...
....
Malizia mwenyewe!
P
Watu wanashindwa kabisa kuelewa ,Uchaguzi unafanyika kabla ya kupiga kura ,wameshasahau mambo ya DC wa Long'ido aliyeweka wazi wanayofanya misituni? Si aliwaambia kwamba uchaguzi wa 2020 hakuna aliyefanya kazi ,kazi yote walikuwa washaimaliza.

Ndiyo maana CDM wanasema No reform ,No election ,Uchaguzi wowote utakaofanyika kwa mazingira yale yale basi upinzani ni za Uso tu mwanzo Mwenga.
 
ni kweli hiyo ni silaha mbaya sana dhidi ya wapenda haki
 
Propaganda ya wa pinzani kuleta vita ilikuwa inatumiwa zamani na CCM baada ya wananchi wengi kuelimika CCM walisha acha kuitumia,siku hizi wanapiga kura nje ya vituo kabla ya siku ya kupiga kura,Siku ya kupiga kura inapofika wanapewa wasimamizi wa vituo kutoka tume ya uchaguzi na polisi ambao wanazijaza kwenye masanduku ya kupigia kura wakati kura zinaendelea kupigwa.
 
Nani kakwambia Tanzania wapo wapinzani wa kisiasa?
hawa waliopo ni mamluki wa CCM
 
Kuna mzee mmoja ambaye ni mzee sana na anaishi kijijini na mwenye elimu ndogo alisema kuwa hiyo silaha wanaifahamu na maana yake wao ndio wataleta vurugu kwani iweje wapinzani wakishindwa hawaleti vurugu eti wakishinda ndio walete vurugu. Na vurugu itaanzia pale watakaposhughulikiwa kwa mujibu wa sheria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…