Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Gentleman,Sikumbuki tarehe ila ilikuwa kati ya mwezi wia 9 au wa 10 hivi 1995 nikiwa na miaka 8 hivi kwenye kitongoji chetu walikuja watu waliovaa nguo za kijani na njano wakitokea wilayani kuja kutuwekea muziki na kisha baadaye kuanza kuongea.
Wale watu nilikuja kuwakumbuka baadaye kidogo nilipokuwa . Ni viongozi wa CCM wilaya kwa ngazi tofauti.
Mama mmoja ambaye yuko hai mpaka sasa mweupe alipopewa mike kuongea alijifanya kuongea kwa uchungu sana kuwa watu wasipochagua CCM ikitokea vita watakaoteseka zaidi ni akina mama, watoto na wazee.
Hii silaha nimeona ikitumika kwenye kila kampeni.
Na upinzani umeshindwa kujibu ingawa majibu yake yalipaswa kuwa mepesi kabisa.
CCM ifike wakati muwahurumie wananchi.
Ilani bora zaidi ya Uchaguzi ya CCM na utekelezaji wa ahadi kwa muaminifu mkubwa ndio pekee mambo yanayowafanya waTanzania wote kuipenda CCM, kuiamini na kuendelea kuipa dhamana ya kushika dola, kuunda serikali na kuongoza Taifa letu.
hivi gentleman,
kweli kabisa uende mbele za waTanzania waerevu, wachapakazi hodari, wanaofanya kazi na majukumu yao ya kujipatia kipato kwa amani, uje uwaambie eti no reform no elections, halafu wakuchague uwe kiongozi wao kweli?
yaan wache kazi zao wababaike na utapeli wako wa aina hiyo, surely?🤣