Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Mkuu, Marekani hadi sasa hawana hayo makombora, kama hujui. Wanajaribu kutengeneza, lakini bado hawajafanikiwa.

Ironically. yule kiduku wa Korea Kaskazini tayari anayo!
labda kama unaizungumzia marekani ya kazimzumbwi.
 
Uko well informed brother
 
Kwenye masuala ya ulinzi una safari ndefu sana kama unakaa hapo unaamini North Korea wana hypersonic missiles. Na umekosea mengi hata kwenye uzi huu, kuna sekta zako unafanya vizuri ila hii unaamini mambo yasiyokuwepo
Mimi nimemjibu nikaishia kuambiwa sijui kitu,..N.Korea leo ana hypersonic cruise missiles sijui amezipata lini.
 
You've made my day 😂 😂 😂 ,mkuu nchi yetu ya amani hii.
 
👆
Katunge World Wide unakubaliana na maoni ya huyu mdau?
 
kaka nikutoe shaka, Jeshi letu naamini lipo vizuri na timamu haswa hatakama nchi yetu haipo kwenye machafuko ila naona huwa wana nunua vifaa vya kivita mara kadhaa nika miezi miwili tu iliyo pita au mwezi mmoja nilikuwa na drive kutoka Tegeta nilikutana na foleni ya kufa mtu kupisha Truks zilizo kuwa zime beba vifaa vya kivita yaani sijajua yalikuwa ni maninj yake ma kitu ila ilikuwa abnormal gari zao zilikuwa ni yale ma semi una kuta limeenea njia nzima can you imagine ni nini kilicho bebwa ? achana na porojo za wasio jua [emoji23] jeshi ni moja ya Taasisi nyeri sana katika nchi [emoji119]
 
Dar nao ni mkoa ulioko mpakani
 
Kwa ninavyojua mimi, ununuzi wa silaha za kivita katika majeshi yote duniani ni "SIRI", so hakuna raia anayejua kwamba Jeshi letu JWTZ lina silaha za aina gani kwa sasa na hata baadae. Kwa muktadha huo, huu uzi hauna mashiko.
 
[emoji115]
Katunge World Wide unakubaliana na maoni ya huyu mdau?
In short jamaa kachambua jeshi letu lote,japo kuna tetesi kuwa now day jw wanamiliki pantsir chache hizi bei yake ni Unit cost: US$ 13.15 million–14.67 million na sijajua ni Variants ipi kati ya Pantsir-S (prototype), Pantsir-S1, Pantsir-S1-O (or Pantsir-S1E), Pantsir-S2

Ila kama zipo kweli basi kuna uhai kiasi fran kwenye ulinzi wa Anga sababu hiz pantsir ni medium range zinawamudu majirani zetu
 
Ulianza vizuri ,lakini hapo mwisho Sasa ndio umeharibu, Asante sana jirani
 
👉Urusi imeshapitwa na wakati sana kwenye teknolojia ya vita.👈
Sijui nani kakudanya katika hili mkuu.Sishabikii vita na wala sipendi vita,kwa kuwa ni mbaya!Ila taarifa recent nilizo nazo ni kwamba Urusi iko mbele ya US in for example nuclear warfare and Supersonic ICBMs.Ni hivi juzi tu ambapo Urusi wame-unveil the SARMAT,an ICBM ambayo ina uwezo wa kubeba up to 15 nuclear warheads, na ni supersonic.Speed yake ni march 20.7,na ina range ya up to18,000km!The US can only dream of such a weapon.Mpaka sasa hawana supersonic missile yeyote ambayo haiwezi kuwa detected.
 
Hilo swali lako nimeshalijibu huko nyuma. Siyo Urusi tu yenye makombora hayo, in fact wako nyuma ila wanajitangaza na kutoa vitisho wakati wenzao hawatangazi. Urusi inategemea sana vitisho kuliko uhalisia wenyewe. Hata kwenye huu uvamizi wa Ukraine walitegemea kwamba Ukraine ingeanguka kutokana na vitisho lakini wakakwama. Juzi juzi wakati Finland inasema inanuia kujiunga na NATO, Urusi ilikatoa vitisho kuwa ittawachukulia hatua wakifanya hivyo, lakini baada ya Finland kutuma maombi yake rasmi NATO kikwelikweli, Urusi wakanyanamaza hao na vitisho vikayeyuka. Mwanzoni mwa uvamizi a Ukraine Putin alisiskika akitoa vitisho vwa silaha za nyukilia kama vile urusi ndio wanazo tu, ambazo kimsingi huwa hazina mshindi. Kwa hiyo usibabaishwe na matangazo ya Urusi kuhusu silaha hizo, ni propaganda tu.

Mwishoni katika technologgy ya vita siyo hayo makombora; kazi ya hayo makombora ni uharibufu lakini hayo siyo yanayoshinda vita. Nchi kama Tanzania haiwezi kununua hayo makombora kwa sababu kwanza siyo mengi, hata urusi na marekani wenyewe wanayo machache tu. Halafu huhitaji gunners maalumu ambazo zimejengewa kwenye meli zao za kivita. Kwa hiyo Tanzania inapotafuta silaha kama vifaru na Howitzers; wasitafute urusi.
 
Bila shaka sasa umekwishajiridhisha kuhusu upotofu wa mada yako nzima kutokuwa na ukweli.

Hizi silaha zinazounguza 'drones' na nyingine zinazopofusha 'satellites' bila shaka zimekwishakufikia hapo ulipo.

Tafuta silaha iitwayo "Zadira", ambayo inachoma madrone, umbali wa kilometa tano, ikitumika tayari kwenye hiyo vita ya Ukraine.

"Peresvet" yenyewe inapofusha satellites umbali wa kilomita 1500 zisiweze kuona kinachoendelea kwenye uwanja wa mapambano. Na bado kuna zaidi ya hizo.

Kwa nchi kama Tanzania nadhani ni muda sahihi wa kuanza kufikiria kama vihela vyetu kidogo vinatumika sahihi kuendelea kununua hizi silaha tunazonunua ambazo tayari zinakuwa 'obsolete'.

Pengine lingekuwa jambo la maana zaidi kuwekeza katika kuwawezesha vijana wetu katika kuwapa ujuzi wa kutafiti katika teknolojia mpya zinazohusiana na silaha ili kujijengea uwezo wa kutengeneza sisi wenyewe tunachoona kinafaa kwa ulinzi wetu.

Hata hivyo, sisemi tujiachie kabisa hata vinchi vya jirani vinavyoonekana kuwa korofi vije vituvamie na tushindwe kabisa kujitetea.
Tusiweke malengo yetu katika kujenga jeshi la kupambana na wakubwa wa dunia, kwa sababu uwezo huo hatunao, badala yake tujikite katika kujiandaa sisi wenyewe kujilinda, hata dhidi ya hao wakubwa huko mbeleni tukishajijenga ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…