Simai kujiuzulu ni ushujaa mkubwa kama Nyerere alivyojiuzulu U-PM. Anastahili pongezi, lawama, shutuma, na kukaliwa vikao au apewe maua yake?

Iltakiwa kuwe na serikali ya mpito miezi mitatu baada ya,JPM kufariki. Hapo watu wangegombea na kuuza sera zao. Anayekubalika zaida anapewa mamlaka, mandate anachagua watu wake.

Majaliwa, Bashiru, Polepole, Lissu, Rungwe, Lukuvi, Samia ,Cheyo wangeuza sera zao. Nchi ingechagua mmoja.

Vitu vya kurithi huna uchungu navyo kuliko vitu ulivyovitafuta na kuwapa ahadi wananchi.

Umeme usingekuwa tatizo nchini angekuwepo JPM, migogoro ya ardhi, polisi, mahakama ingepungua pamoja na madhaifu yake mengine alikuwa na nia ya dhati kulikomboa hili taifa.
 

Ila nimekuelewa vizuri. SSH angekuwa mzalendo ingebidi ajiuzulu baada ya miezi mitatu. Aitishe uchaguzi mpya, huru at least ndani ya chama chake.

Ndugai hakufanya makosa yoyote. Lukuvi, Kabudi, Polepole , Kalemani, Majaliwa, Jaffo wote wamefukuzwa kwa unafiki, majungu, kiaina.

SSH Angeshinda ndio angeteua baraza lake la mawaziri.

Naona kampeni zake zingekuwa nafukuza viongozi wazuri wote, hamtapa, umeme, maji, sukari 5000, timua machinga,choma masoko, uza Ngorongoro, bandari, misitu.

Holiday kila mwezi labda angeshinda.
 
Mleta mada, Makonda unamuona ana boldness? Kipimo chake subiri 2025 ccm wakiiba kula za uchavuzi kama atajiuzuru. Akiweza hili, nitamweka kwenye kundi unalolisema wewe.
Kwa sasa yupo kwenye kundi la vijana wajanja wanaojua kuzichanga karata ili kupata wakitakacho huko mbeleni, ni hatari kupewa nyazfa za juu za nchi
 
Tumekusikia na kukuelewa. Ila Mkuu hapo namba 5 kuna kitu kimejificha. Nacho ni sababu za aliyekuwa PM wa wakati huo kujiuzuru kwa hiari yake. Upatapo nafasi funguka zaidi kwa manufaa ya kizazi cha sasa.
Wasalaam.
 
Kwa jinsi unavyojieleza hapo juu, ukiujua ukweli hutaamini kabisa.
 
Unapokiri Nyerere alirekebisha mengi aliyokosea awali, halafu tena bado unaendelea kutumia maneno "nguvu na utukufu" unaonesha vile usivyojua maana ya kile unachoandika.

Kama Nyerere angekuwa anapenda unachoita "nguvu na utukufu" simply asingefanya marekebisho yoyote, ili aendelee kufaidi hicho unachoita "nguvu na utukufu".

Lakini kwa marekebisho aliyofanya unayokiri mwenyewe, na pale alipotamka Katiba yetu inaweza kumfanya Rais awe dikteta, lakini yeye akaamua kun'gatuka, kunazidi kuonesha usivyojua maana ya "nguvu na utukufu".

Pia, hata ukilazimisha kuita "FACT", ukweli ni kwamba hiyo "FACT" yako haina maana, simply umeamua kujiliwaza tu na maneno yaliyokosa uhalisia, tena yanayopingana na maelezo yako mwenyewe ya awali.

Nyerere kujiuzulu uwaziri mkuu ili kwenda kuwa Rais, alifanya vile ili kukamata hiyo post ambayo mwanzo haikuwepo, kulazimisha kusema alifuata "nguvu na utukufu" ni kujifurahisha tu mwenyewe, utukufu na nguvu zipi ambazo mwenyewe aliziacha bila kushurutishwa na yeyote? na akatuachia rasilimali zote kama zilivyo?!

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Pumbavu miaka 24 aliyokaa nyerere ni midogo? Mambo yalimshindal nyerere ndipo akamshushia zigo mwinyi
 
Mwinyi mzushi tu kama ilikuwa kweki anamaslahi si angempiga chini.
 
Pascal Mayalla bandiko lako halijitisholezi kwa kueleza 'dhana' ya kujiuzulu na si kwanini Simai apewe 'ushajaa'
Ningeshauri ueleze kwa kina kwanini alijiuzulu na kwanini hatua hiyo imekuwa nzuri.

Rais A.H.Mwinyi alijiuzulu kwa kashfa ya mauaji ya Vikongwe akiwa Waziri ili kulinda heshima ya Bosi wake.

Simai amefanya kipi ?

Bila kufafanua ipo siku Waziri atajiuzulu kwasababu tu amehisi habari za mchepuko zitavuja, naye tumwite shujaa kwasababu tu amejiuzulu! Ushanfaham mkuu!

JokaKuu
 
Pascal Mayalla. Kujiuzulu Tanzania sio lazima uwe wewe umeamua, unaweza kuamuliwa na kuambiwa saini hapa umejiuzulu au ....

Ukishaini wanasema njoo upige picha, utoe tamko.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…