Simama upande wa Lulu

Simama upande wa Lulu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Kama binadamu na Kama mzazi ukiacha mapungufu yote ya Lulu. Elizabeth Michael naye ni binadamu mwenye hisia kama wengine! Anastahili kupata kila unachostahili wewe, upendo ulinzi kujaliwa utu wake kusifiwa privacy nk nk
Kuna watu wana kipawa cha kuwa maarufu kiasili Lulu ni mmojawapo na tatizo limeanzia hapo

Ni binti ambaye nyota yake iliwaka akiwa mdogo kabisa, umaarufu wake kuna watu wameusotea miaka bila kuupata..hili ni tatizo la pili

Nyota yake hiyo ikaenda sambamba na matatizo, katika Umri mdogo kabisa akapata mpenzi ambaye mamilioni ya wanawake wangetamani kumpata na ikibidi kummiliki milele..hili ni tatizo la tatu na msingi wa mada

Hulka yake binadamu ni kufurahia ama kuona mwingine anashindwa hasa yule anayedhani kamzidi hiki ama kile...ishu za haters huanzia hapa

Tangu wakati huo Lulu hajawahi kupumua ikawa ni bandika bandua ya matatizo, sehemu kubwa ya jamii ikajitenga naye bila kutafakari kwamba nje ya ustaa na umaarufu wake Lulu ni binti kama binti mwingine yoyote anayepitia hatua za kawaida kabisa za makuzi na anakumbana na mengi....

Mabinti wengi huchukua maamuzi mabaya ya kujiua kwenye changamoto ndogo tu za ukuaji. Jamii ikamtenga fulani hivi wachache wakampa moyo wa kusonga mbele anaweza kusimama na kuendelea mbele NAMSIFU

matatizo yamemkomaza yuko imara kuliko maelfu ya watu, lakini ni nani anayependa kuambiwa kuwa ana nuksi? Ama kimavi? Ni nani anayependa kuitwa kuwa yeye ni malaika wa kifo? Hakuna!!!!

Lulu katika binadamu wake anapenda maisha yake amani furaha na upendo... Lakini kagundua kuna tatizo mahali... Kaenda kusaka tiba mbadala, limekuwa ni tatizo kubwa!

Ni nani ambaye hapendi kujaribu njia nyingine kama akiona mambo hayaendi? Tuacheni unafique kiwango cha PhD
 
Mbona ndugu zake warombo hawasumbuliwi?sense akaishi kwa baba yake. Maisha ya kawaida.
Yeah kwakuwa wao si yeye kila mmoja ana mustakabali wake, muunganiko wa damu hauzuii kuwa na maisha tofauti
 
Yeah kwakuwa wao si yeye kila mmoja ana mustakabali wake, muunganiko wa damu hauzuii kuwa na maisha tofauti
Huyo mpenzi wake ni wa kike au wa kiume?! Au ni mpenzi mwenye dushe ambalo peke yake halikidhi kuitwa mwanaume....
 
Ni suala la kujiuliza. Kwa yale uliyopitia, uki-assume ungekuwa maarufu na kila mtu angeyajua; je ungeonekana una bahati? Au mapepo?
 
Lini umehamia huku mdogo wangu? Huyu binadamu nilikutana naye ATM pale CRDB masaki alinipiga kikumbo karibu nidondoke bahati mimi ni pande la mtu. Ukiwa na jina jiheshimu na heshimu watu utaheshimika.
[emoji3] [emoji3] pole dada Msamehe tu maisha yameshape awe hivyo alivyo sasa
 
[emoji3] [emoji3] pole dada Msamehe tu maisha yameshape awe hivyo alivyo sasa
Hahaha umeshafika bongo? Hawa watu wanajisahau ila si wao tu dunia iko vile. Ukisotea nafasi unaiheshimu ukiiokota na wewe unaokoteleza misifa.
 
Hahaha umeshafika bongo? Hawa watu wanajisahau ila si wao tu dunia iko vile. Ukisotea nafasi unaiheshimu ukiiokota na wewe unaokoteleza misifa.
Nipo dada since last week lakini pembeni kidogo VP umeshaondoka?

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom