mlinzi mlalafofofo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2008
- 725
- 1,282
Miaka fulani uko nyuma nikiwa mkoani kwangu nilishuhudia uwanja mkubwa ulio jirani yetu ukisafishwa na bdae palifanyika ujenzi matata kabisa mahala pale.
Kwa harakati zilizokuwa zinaonekana pale ni wazi walikuwa wanajenga kitu kikubwa sana km hoteli kubwa au kitu kinachofanana na hicho.
Kwa nyepesi za pale kitaani kwetu huyo mmiliki alikuwa anaishi dar, hapa nitamwita "boswadaa". sasa cha ajabu boswadaa yeye alikuwa akituma pesa tu bila yeye mwenyewe kuja kule mkoani kuona yanayoendelea kwenye saiti yake. Alikuwa na jamaa zake anaowaamini pale mkoa ndio kama wasimamizi japo nao walikuwa hawana hata huo muda wa kufika hapo saiti. sanasana kama wakija wanakuja kununua/kuchukua mifuko ya simenti ya boswadaa na kutokomea zao. Kwaiyo wale mafundi ni km walikuwa hawana mabosi wa kuwasimamia. utawala wa manyani kila mtu yupo frii afanye anavyotaka.
Ile saiti ikageuzwa kuwa sehemu ya kununua matirio hasa zile simenti zilizokuwa zinaletwa na boswadaa. mzigo ukiingizwa mlango wa mbele unatolewa kule milango ya nyuma. Wanunuzi walifurahia wakidai simenti ya boswadaa ilikuwa beichee ni sawa na bure tu.
Kila siku ile saiti ilifurika wananzengo wakivizia fursa ya kununua mzigo wa simenti wa bei chee wa boswadaa.
Sisi wengine wkt mambo haya yanafanyika hatukuwa na la zaidi la kufanya zaidi ya kusikitika na hasa kumsikitikia boswadaa na zaidi tukishangaa kwanini yeye mwenyewe haonekani saiti hata kwa masaa machache kuona maendeleo ya mradi wake. tukaganga na yetu.
Jumba lile halikuweza kukamilika na hata sasa baada ya miaka mingi kupita, jengo lile ni gofu la kucheza panya na mijusi. ndoto ya boswadaa kumiliki hotel ni km imetamatishwa, japo mjadala utabaki ni nani aliyetamatisha ndoto hizo kati ya boswadaa mwenyewe au wale aliowaamini wangeweza kumsaidia usimamizi.
Bandugu tujihadhari na huu ujenzi wa simu au usimamizi wa ndugu, jamaa na kama ni lazima basi hakikisha unapata muda wa kufika au kujua kinachoendelea saiti, maana hata wale unaowaamini wanaweza kukuangusha kama walivyomfanya huyu boswadaa.
Ujenzi huu ninaousimulia hapa haukuweza kukamilika na pengine huyo mhusika alipoteza pesa nyingi sana maana ni km alikuwa akitumbukiza pesa kwenye shimo lisilo na mwisho hadi kashindwa kusimama tena.
Wewe uliyefanya mradi ule miaka ile ktk mkoa X kama leo hii unasoma hapa jua kuwa haya ndiyo yaliyotokea kwenye mradi wako ule na wale uliowaamini kusimamia walikuwa hawasimamii na sanasana walikuwa sehemu ya kukudimiza maana nao walikuwa wateja wazuri wa simenti zako.