Wale mnaosema hakuugusa, msikieni goalkeeper wa prisons ambaye alikuwepo eneo la tukio
View attachment 2106972
NIMEPOKEA HII TAARIFA KUTOKA KWA OC CHANIKA, INAWEZA KUWASAIDIA.
Anawapasha wapelelezi na askari wote na pia anaomba ku-share nao mbinu mojawapo inayotumiwa na wahalifu katika kufanikisha wizi kwa njia ya mtandao. Huu ni uzoefu alioupata baada ya mahojiano na mtuhumiwa mmojawapo wa kesi ambayo ASP LEOFORD, OC- CID Simanjiro ametuma simu kwenye group muda mfupi uliopita kwa OC Chanika kutuma escort kwenda kuchukua mtuhumiwa.
Katika tukio hilo, kuna mtu aliibiwa simu na siku moja baadae ikafanyika miamala ya kuhamisha fedha kutoka kwenye account yake ya M-Pesa kiasi cha zaidi ya TZS. 3,000,000/= kwenda kwenye namba tofauti za simu. Swali ambalo wengi wangependa kujua ni kwamba, mwizi huyo aliwezaje kujua namba ya siri ya aliyeibiwa simu hadi kuweza ku- access account yake ya M-pesa na kutoa fedha??!!
Wengi wetu wanaweza kusema watu wa kampuni za simu wanahusika katika hili. Hebu fuatilia ujue mbinu iliyotumika au inayotumiwa na wezi wa aina hii:
1. Simu ikishaibiwa, kama simu yenyewe ina password, wanatoa line na kuweka kwenye simu nyingine.
2. Hatua ya pili, mwizi atataka kujua line hiyo ya simu imesajiliwa kwa jina gani? Hivyo atapiga *106# na baada ya hapo atabonyeza No 1. Kama line imesajiliwa, atakuwa amepata kujua jina kamili la mmiliki wa line hiyo.
3. Hatua ya tatu, atataka kufahamu account ya mwenye simu, mfano: m-pesa, ina kiasi gani cha fedha? Hapo mwizi atatumia simu yake au simu ya mtu mwingine anayefahamiana naye kutuma kiasi fulani cha fedha, mfano atatuma TZS. 2,000/= kwenda kwenye namba ya simu ya aliyeibiwa. Pesa hiyo ikishaingia, automatically line ya simu iliyoibiwa italetewa sms inayoonyesha kutumiwa kiasi cha fedha, na salio lake jipya la wakati huo baada ya kutumiwa fedha.
4. Baada ya mwizi kujua salio, sasa anaweza kuweka mikakati ya kuiba kama account ya aliyeibiwa simu ina kiasi cha fedha zinazoweza kuibika.
•Hatua ya kwanza anapiga simu Customer Care na kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye line ya simu iliyobiwa. Kumbuka jina analo tayari.
•Hatua ya pili akishapiga simu, atawaambia kuwa amesahau password ya account yake,
Customer Care watakachotaka kujua kutoka kwake ni lini alifanya muamala wa mwisho, na ilikuwa ni kiasi gani, na salio lake kwenye account yake ni kiasi gani. Kumbuka taarifa zote hizo jamaa anazo tayari, hivyo anawaelezea watu wa Customer Care na wanamuelewa vizuri tu.
•Kutokana na usahihi wa taarifa za mwizi alizotoa kwa Customer Care, watamuamini na kumtumia code namba ambazo atatumia kubadilisha namba ya siri, na hivyo anafanikiwa ku-access account ya victim na kufanya miamala vile atakavyo.
MUHIMU
Ni vyema ikitokea mtu kaibiwa simu yake, immediately apige simu kampuni husika na kutoa taarifa ili line yake iwe blocked. Asitumie muda mrefu kutoa taarifa polisi na kufuatilia Loss Report pasipo kwanza kuwasiliana na Service Provider. Hii inaweza kusaidia kuzuia madhara yanayoweza kutokea mara baada ya mtu kuibiwa simu. Asanteni
From: OC Chanika, Asp. Nyambalya
Nawasilisha tafadhali. Tusaidiane Ku Share taarifa hii ili kulipa sarport Jeshi letu la Polisi ambao kila kukicha hawalali, wakitulinda sisi raia pamoja na mali zetu dhidi ya wahalifu.