Wakuu nimesikia tetesi kwamba Kocha wa 2020 - 2021 Pablo Flanko Martine yupo Tanzania. Pablo alikuwa akizira zira, alikuwa akigombana na akina Wawa, anapigapiga Machupa, hajawahi kuwa na ubingwa wowote. Na limpira lake la kukimbia kimbia.
Kuna tetesi kwamba huenda akamalizana na Uongozi wa Simba kurudi kibaruani kama Kocha Mkuu.
Kumrudisha Huyu mtu ni kwenda kujihakikishia kushika nafasi ya tatu.
1. Yanga
2. Azam
3. Simba
Tujiandae kisaikolojia.
Ushauri
Ningetamani sana Simba wamrudishe Didier Gomez Darosa. Huyu ni moja kati ya Makocha wangu bora kabisa kuwahi kuwaona Tanzania. Ila kiherehere cha kumtoa Simba kwa uzembe wa Wawa kwenye mchezo wa Jwaneng Galax.
Kulikuwa na tetesi kuwa Simba imemalizana na kocha wa Vipers ya Uganda, Mabingwa wa soka nchini Uganda Robertinho Oliviera.
Kocha huyo ambaye amekuwa na msimu bora na klabu hiyo ya nchini Uganda na inaelezwa amewavutia mabosi wa Klabu ya Simba miamba hiyo ya soka nchini Tanzania. Kocha wa Vipers ni mzuri, ikishindikana Gomez.
NB: Simba waache ushamba wa kubabili makocha.