Kweli wewe mbumbumbu,kipindi hicho cha Simba anaingia fainali kulikuwa na mshindano matatu ya CAF;
1. Champions Cup ambapo hii ndio Club Bingwa ya sasa,Tanzania iliwakilishwa na Malindi ambae ndie aliekuwa Bingwa wa Kombe la Muungano. Fainali ilichezwa kati ya Asante Kotoko ya Ghana vs Zamalek,Zamalek akawa Bingwa.
2. Kombe la Washindi Barani Africa,ambapo ndio Kombe la Shikirikisho kwasasa,Tanzania iliwakilishwa na Pamba ya Mwanza baada ya kuwa Bingwa wa FA Cup ambayo ilikuwa inaitwa Nyerere Cup kipindi hicho,fainali ilichezwa kati ya African Sports vs Al Ahly ya Misri,Bingwa akawa Ahly.
3. Kombe la CAF Cup ambalo hili lilianzishwa na mwanasiasa mashuhuri nchini Nigeria Mashud Abiola ambapo Tanzania iliwakilishwa na Simba,na Stella Adbjan akawa Bingwa. Abiola alipouawa na kombe likafa.